Home Kitaifa Mwadui yachafua daftari la Manula

Mwadui yachafua daftari la Manula

7886
0
SHARE

Rekodi ya Aishi Manula kutoruhusu goli kwa michezo sita mfululizo ya ligi kuu imeishia kwa Mwadui ambao wameivunja rekodi hiyo kwa kumtungua mabao mawili walipoilazimisha Simba sare ya kufungana 2-2 kwenye uwanja wa Kambarage, Shinyanga.

Mechi sita alizocheza Manula bila kufungwa ni sawa na dakika 540, kabla ya mchezo wa leo golikipa huyo wa Taifa Stars aliruhusu goli kwenye mchezo dhidi ha Lipuli uliochezwa uwanja wa Uhuru goli ambalo lilifungwa na Asante Kwasi wakati huo akiichezea Lipuli.

Ni mara ya pili Manula anaruhusu magoli mawili ndani ya mechi moja, mara ya kwanza kufungwa magoli mawili kwenye mchezo mmoja ilikuwa Septemba 21, 2017 Simba ilipojikuta inang’ng’aniwa kwenye uwanja wa CCM Kirumba na kulazimishwa sare ya kufungana 2-2.

Manula ameidakia Simba mechi 18 za VPL hadi sasa na kuruhusu magoli nane (8) ambayo ni magoli machache kwa magolikipa waliokaa golini katika mechi 18 tangu kuanza kwa msimu.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here