Home Kitaifa Mkude lawamani sare ya Simba Shinyanga

Mkude lawamani sare ya Simba Shinyanga

16128
0
SHARE

Baada ya Simba kulazimishwa sare ya kufungana 2-2 na Mwadui mkoani Shinyanga, baadhi ya mashabiki wametupa lawama zao kiungo wao Jonas Mkude ambaye aliushuhudia mchezo huo akiwa ndani ya gari.

Taarifa zilizopo ni kwamba Mkude alichelewa ndege waliyoondoka nayo wachezaji wenzake na benchi la ufundi kuelekea Mwanza na baadaye Shinyanga kwa ajili ya mechi ya iliyochezwa leo.

Kitendo cha Mkude kutowekwa hata kwenye benchi la wachezaji wa akiba kimetafsiriwa tofauti na mashabiki wa Simba pamoja na timu nyingine. Jambo hilo linadhaniwa pengine huenda ni maamuzi ya benchi la ufundi kumtosa Mkude ili kujenga nidhamu ya timu.

Mchezo ulipomalizika baadhi ya mashaki walipaza sauti zao wakihoji kwa nini Mkude hakupangwa kwenye mechi hiyo lakini pia wapo waliounga mkono kwamba ni lazima ‘atiwe’ adabu iwe fundisho kwake na vizazi vingine.

Mkude amekuwa kwenye kiwango cha juu siku za hivi karibuni baada ya kupata nafasi kwenye kikosi cha Simba kufuatia kuondolewa kwa Joseph Omog kama kocha mkuu wa Simba

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here