Home Kitaifa Yanga wanamkimbiza mnyama kimya kimya…MajiMaji wapigwa 4

Yanga wanamkimbiza mnyama kimya kimya…MajiMaji wapigwa 4

8148
0
SHARE

Yanga imeendelea kushinda mechi zake za ligi kuu Tanzania bara licha ya wachezaji wake wengi kuwa nje wakiuguza majeraha, leo Jumatano Februari 14, 2018 imepeleka salamu za Valentine kwa mashabiki wake kwa ushindi wa mabao 4-1 dhidi ya Majimaji.

Ushindi dhidi ya Majimaji ni wa tano mfululizo kwa mabingwa hao watetezi wa taji la VPL, huku ukiwa ni ushindi wao wa sita katika mechi sita zilizopita.

Yanga imefikisha pointi 37 zinazoifanya ijiimarishe kwenye nafasi ya pili ikiiacha Azam kwa pointi tatu baada ya timu hizo kucheza mechi 18 kila moja. Yanga inaendelea kuifukuza Simba kwenye nafasi ya kwanza kwenye msimamo wa ligi ikiwa nyuma kwa pointi tatu, wekundu wa Msimbazi wana pointi 41 lakini wanasubiri kucheza kesho ugenini dhidi ya Mwadui.

Majimaji hali yao inaendelea kuwa mbaya wakiwa nafasi ya pili kutoka mwisho (15) kwenye msimamo wa ligi kwa pointi zao 14 baada ya kucheza mechi 18. Pointi hizo ni sawa na Njombe Mji na Kagera Sugar.

Majimaji imefungwa magoli nane kwenye mechi mbili walizocheza uwanja wa taifa (Simba 4-0 Majimaji, Yanga 4-1 Majimaji), huku yenyewe ikifunga goli moja pekee.

Kabwili ameruhusu goli moja katika mechi tatu alizocheza. Aliingia akitokea benchi kuchukua nafasi ya Youthe Rostand ambaye aliumia kwenye mchezo dhidi ya Lipuli uliomalizika kwa Yanga kushinda 2-0.

Alidaka kwa mara ya kwanza kwa dakika 90 mchezo wa VPL Yanga iliposhinda 4-0 dhidi ya Njombe Mji, akacheza mechi ya kimataifa na kuendeleza clean sheet Yanga ilipohinda 1-0 dhidi ya St Louis lakini Majimaji wamemtibulia rekodi yake.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here