Home Kimataifa Real Madrid vs PSG kuisimamisha dunia kwa dakika 90

Real Madrid vs PSG kuisimamisha dunia kwa dakika 90

7322
0
SHARE

Leo ni vita ya pesa kati ya matajiri wawili Real Madrid watakaowakaribisha Paris Saint German huku rekodi ya michezo yao iliyopita ikionesha kwamba kila timu imeshinda mara mbili nanpia wametoka suluhu mbili.

Msimu huu kati ya malengo makubwa ya matajiri wa Paris Saint German ni kubeba Champions League lakini katika mashindano matano ya Champions League yaliyopita PSG hawajawahi kupita kwenda robo fainali.

Lakini wakati PSG wakihangaika kuitafuta robo fainali, hali kwa wenzao Real Madrid ni tofauti kabisa kwani mabingwa hao watetezi katika mashindano saba yaliyopita ya Champions League wamefanikiwa kufudhu kwenda nusu fainali.

Santiago Bernabeu sio salama kabisa kwa mpinzani yeyote anayekanyaga kwani katika michezo 10/14 iliyopita Real Madrid walipata ushindi chini ya Zinedine Zidane na michezo yote 6 katika uwanja wa Santiago Bernabeu waliibuka kidedea.

Katika hatua kama hii ya mtoano PSG wamepoteza michezo minne kati ya sita ambayo wamecheza ugenini lakini msimu huu rekodi yao ya ufungaji inaogopesha sana kwani wameshaweka kambani mabao 25 katika hatua ya magrupu.

Kwa Gareth Bale huu unaweza kuwa mchezo wake muhimu kabisa kwani kama atakuwepo uwanjani hii leo baasi atakuwa amefikisha michezo 50 ya Champions League na kufikia rekodi ya Ryan Giggs kuwa mchezaji wa Wales wa pili kufikia idadi hiyo ya michezo.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here