Home Ligi EPL Mwacheni Pogba kama alivyo

Mwacheni Pogba kama alivyo

10963
0
SHARE

Na Priva ABIUD

Hali ya Man United ni ngumu sana. Maisha yamewabadilikia sana. Jana nilibahatika kuongea na mzee mmoja wa miaka kama 70 hivi. Nikamuuliza vipi Man United imewahi kuwa na wakati mgumu kama huu? 

Mashabiki wengi wa United naona kama wanasubiria Meli Dodoma. Kwanza wameanza kufarakana wenyewe kwa wenyewe kimawazo. Wapo wanaoamini Kuna Masihi Mwingine atakuja na wapo wanaomini kuwa masihi ni huyu huyu. Masihi ninaemzungumzia ni Nani? Ni Paul Labile Pogba. Hivi majuzi ulizuka mjadala mzito kuhusu Pogba Na Kevin Debruyne. Niliwaambia Mashabiki wa Man United waachane na hisia mkurupuko. Debruyne sio wa kufananishwa na Pogba. Wengi wao walinitukana na kusema namba hazidanganyi.

Yule mzee alinijibu kuwa kwa kipindi cha miaka 20, Haijawahi kutokea Man United mbovu kama hii ya kuanzia 2013 mpaka sasa. Man U ya sasa ni mbovu haswa. Anasema kwanza wanacheza mpira wa maji taka. Nikamuuliza mbona kipindi cha nyuma Ferguson Alex alikuwa sio muumini sana wa pasi nyingi na ukiachilia mbali haikucheza vizuri sana lakini timu ilipata mafanikio makubwa?

Niliwahi kusema kuwa debruyne sio wa kufananishwa na Pogba. Debruyne ni ebola pogba ni kikohozi. Masihi wao ndo huyu huyu. Wala wasitegemee kikubwa zaid ya hiki wanachokiona kutoka kwa Pogba. Pogba wa Juve ndo huyu huyu wala hawana tofauti. Shida sio takwimu. Sio kila takwimu zinaashiria uwezo wa mchezaji. Ila ufanisi katika nafasi unayocheza na mfumo uliotumika.

Yule babu akaniambia Usifananishe kifo na usingizi. Man United haijawahi kucheza vibaya kama hii. Akasema, “ukisema Man United ilicheza vibaya unataka kuondoa uwepo wa Scholes kwenye Historia ya soka, Unataka kutumbia Ronaldo alikuwa zwazwa? Ni sawa na kusema Hukuwahi kuona kizazi cha akina Giggs cha miaka ya 90 kikicheza? Akaniambia Man United ya Zamani ilicheza mpira wa kushambilia zaidi kwa kutumia mawinga. Haikuwa inacheza mfumo wa kukaba. kushambulia ndiko kulikuwa lengo la kwanza, ila ya sasa kuzuia ndo lengo msingi. Akamalizia kwa kusema Man United ya sasa inacheza kama Konokono.

Wapo wanaosema Pogba alikabiwa na wachezaji wawili nyuma yake. Huwa nachekaga sana. Wanakwambia Vidal na Pirlo walimkabia Pogba. Labda niwaambieni kitu, Msimu uliopita pogba amecheza Mbele ya Carrick na Herrera (Wote wanakaba). Vidal sio kiungo mkabaji kiasilia nidhamu yake ya ukabaji ni mbovu huwezi kumfananisha hata na Herrera. Naheshimu nafasi ya Pirlo katika soka, natambua uwezo wake lakini jukumu lake kuu hakuwa kiungo mkabaji. Sasa nataka niwaulize mlimaanisha nini? Hata  Marchisio sio Kariba ya Akina Ngolo Kante. Naombeni niwaulize mliaamnisha Pogba hawezi kucheza bila wachezaji wazuri nyuma yake? Kwahiyo Pogba anategemea wachezaji wazuri pekee ili afanye vizuri? Kwanza pogba alicheza kama kiungo wa katikati kushoto na kiungo mkabaji miaka yake ya Juventus. Ni mara chache sana alicheza kama namba 10 kama wengi mnavyodai kuwa anapaswa kucheza hiyo nafasi.

Kwahiyo Pogba hawezi kucheza bila Vidal na Pirlo? Kama ni hivyo basi mlidhulumiwa milioni 90. Mnamkosea Pogba mnaposema kuwa anategemea wachezaji fulani. Pia mnamtukana Carrick, matic na Herrera kuwa sio wachezaju wazuri. Niwakumbushe kitu. Msimu wa mwisho Pogba kuondoka Juventus ndio aliokuwa na takwimu bora kabisa . Lakini hakucheza na  Vidal, alishakwenda zake Buyern, Marchisio alivunjika karibia Nusu msimu. Marchisio sio kiungo mkabaji mzuri kama Herrera. Pirlo sio mkabaji sana kumzidi Carrick.

Shida iko wapi? Shida ni hela, mfumo na matarajio makubwa. Pesa iliyotolewa na kile mnachoona ni tofauti. Sijui mlidhani atakuja kucheza kama Iniesta. Watu wanataka Pogba awe free. Mourinho alimpa Pogba uhuru huo msimu uliopita. Mnasema Pogba anachotaka ni uhuru wa kupanda na kushuka, je kupanda na kushuka ndo kazi ya namba 10 hiyo? Ukweli utabaki pale pale. Huyu ndiye Pogba. Uwezo wake ni ule ule. Hakuna Pogba tofauti na huyu. Tena huyu wa sasa ana majukumu makubwa na muhimu kuliko Juventus. Pogba wa Juve alikuwa mvulana kwa sasa ndiye mwanaume. Apambane kiume asisubiri vivuli vya watu.

Tukimpa Dereva mzuri gari bovu hatuwezi kusema huyu dereva ni mbovu. Kinachofanya mumtazame Pogba ni matokeo mabovu yanayotokana na malalamiko ya babu. Timu inacheza ovyo. hata huyo Pogba mumpeleka namba 9 bado hawezi kufunga magoli 9 kwa mwaka. Mfumo mbovu unafanya tuone wachezaji hawacheza vizuri. Shida sio Pogba ni mfumo. Shida sio watu ni mfumo. Pogba ni yule yule. Hana kiwango kingine zaidi ya hiki. Vipi lakini mmejiandaje na Valentine.?

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here