Home Kimataifa Liverpool kuendeleza rekodi ya kutofungwa katika Champions League hii leo?

Liverpool kuendeleza rekodi ya kutofungwa katika Champions League hii leo?

5792
0
SHARE

Liverpool wameshakutana na Fc Porto mara nne katika michuano tofauti lakini katika mara zote hizo Fc Porto hawajawahi kuwafunga Liverpool hata mara moja na kama wakifanya hivyo hii leo baasi itakuwa mara yao ya kwanza.

Hii ni mara ya kwanza kwa Fc Porto kufudhu kwenda katika hatua ya mtoano mara mbili mfululizo tangu wafanye hivyo msimu wa 2009/2010 lakini hawajawahi kwenda robo fainali tangu ule msimu wa 2004 ambao walibeba kombe.

Liverpool wanakwenda katika mchezo huu wakiwa na rekodi nzuri sana kwani ni kati ya timu nne ambazo hadi hivi sasa hawajapoteza mchezo hata mmoja katika Champions League msimu huu, timu nyingine ni Barcelona, Tottenham na Besiktas.

Hatari kubwa kwa Liverpool hii leo inaweza kuwa uwezo mkubwa wa Porto kupiga mipira ya “set-piece” ambapo katika msimu huu wa ligi ndio klabu ambayo inaongoza kwa ufungaji wa mabao ya “set-piece” (mabao 8).

Uwanja wa klabu ya PSG “Parc Des Princes Stadiym” ndio uwanja unaoongoza kwa kuzalisha mabao mengi katika CL msimu huu(16) lakini unaofuatia ni uwanja wa Fc Porto “Portos Dragao” (mabao 15).

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here