Home Kitaifa Hesabu za Yanga kwa Simba haziwaachi salama Majimaji

Hesabu za Yanga kwa Simba haziwaachi salama Majimaji

7228
0
SHARE

Leo Jumatano ya Februari 14, 2018 wakati watu wengi wakiwa kwenye shamrashamra za Valentine’s Day, Yanga na Majimaji watakuwa wakisambaza upendo uwanjani kwenye mchezo wa VPL utakaopigwa uwanja wa Uhuru mishale ya saa 10:00 jioni

Mchezo huu ni muhimu sana kwa kila upande (Yanga na Majimaji), umuhimu unakuja pale Yanga wanapozitaka pointi tatu ili kuendelea kuikimbiza Simba kwenye mbio za ubingwa wakati Majimaji pointi tatu kwao ni muhimu ili kujikwamua kwenye nafasi ya mwisho kwenye msimamo wa ligi angalau wasogee juu.

Yanga ina rekodi nzuri ikicheza na Majimaji kwa mechi zilizochezwa Dar, kwa majimaji ni kinyume. Yanga imechukua pointi zote tatu mbele ya Majimaji katika michezo tatu zilizopita jijini Dar.

Majimaji imekuwa vizuri ikicheza na Yanga kwenye uwanja wa Majimaji Songea mkoani Ruvuma, imeokota pointi tatu kutokana na sare tatu kwenye uwanja huo na mupoteza mchezo mmoja tu kati ya mechi nne zilizochezwa dimba la Majimaji.

Mechi 7 zilizopita za VPL Yanga vs Majimaji

 • Majimaji 1-1 Yanga
 • Majimaji 0-1 Yanga
 • Yanga 3-0 Majimaji
 • Majimaji 2-2 Yanga
 • Yanga 5-0 Majimaji
 • Majimaji 0-0 Yanga
 • Yanga 1-0 Majimaji

Gali la limewaka, siku za hivi karibuni Yanga imeshinda mechi nne mfululizo za ligi kuu ikiwa ni mara ya kwanza kwa timu hiyo kushinda mechi nyingi mfululizo ndani ya msimu huu hadi sasa. Jumla Yanga imeshinda mechi tano mfululizo pamoja na mchezo wake wa uliopita wa Caf Champions League dhidi ya St Louis.

Katika mechi tano zilizopita, Yanga imefunga magoli tisa huku yenyewe ikiwa imeruhusu bao moja tu.

Mechi 5 zilizopita za Yanga

 • Ruvu Shooting 0-1 Yanga
 • Azam 1-2 Yanga
 • Lipuli 0-2 Yanga
 • Yanga 4-0 Njombe Mji
 • Yanga 1-0 St Louis

Majimaji tia ‘maji-tia maji’ hawajashinda hata mechi moja ya VPL katika mechi zao tano zilizopita, wameambulia sare mbili huku wakipigwa katika michezo yao mitatu. Wamepata pointi mbili kati ya 15 walizokuwa wanazifukuzia hivyo wamepoteza pointi 13.

Mechi  5 zilizopita VPL za Majimaji

 • Majimaji 1-1 Azam
 • Majimaji 0-1 Singida United
 • Simba 4-0 Majimaji
 • Majimaji 1-2 Mbeya City
 • Majimaji 0-0 Tanzania Prisons

Yanga ipo nafasi ya pili kwenye msimamo wa ligi ikiwa na pointi 34 baada ya kucheza mechi 17 ikiwa sawa kwa pointi na Azam ambayo tayari imecheza michezo 18. Yanga inazitolea macho pointi tatu dhidi ya Majimaji kwa sababu mbili.

1. Ushindi utaifanya iongeze gap la pointi dhidi ya Azam, ambapo itaizidi kwa pointi tatu huku timu zote zikiwa zimecheza idadai sawa ya mechi (18) hivyo Yanga watakuwa mbele ya Azam kwa tofauti ya pointi na sio magoli tena.

2. Yanga itapunguza gap la pointi dhidi ya Simba ambayo itacheza kesho ugenini dhidi ya Mwadui. Endapo Yanga itashinda itafikisha pointi 37 pointi nne nyuma ya Simba inayoongoza ligi ikiwa na pointi 41 huku ikiyarajia kucheza kesho mechi yake ya 18.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here