Home Kimataifa Utemi wa Pep Gurdiola kuhamia kwa Fc Basel hii leo

Utemi wa Pep Gurdiola kuhamia kwa Fc Basel hii leo

4564
0
SHARE

Kama ilivyo kwa mchezo kati ya Juventus Vs Tottenham utakaopigwa hii leo, ndivyo itakavyokuwa kwa mchezo kati ya Basel vs Man City ambao nao utakuwa mchezo wa kwanza baina ya timu hizi katika Champions League.

Watu wengi wanawachukulia Fc Basel kama “under dogs” kuelekea katika mchezo huu lakini uhalisia ni kwamba Basel sio wa kuchukulia poa hata kidogo, michezo yao 5 ya mtoano iliyopita nyumbani vs timu za Uingereza wameshinda 4 na kupoteza mmoja tu.

Na sasa wakati Basel ana rekodi nzuri hivyo, wenzao Man City wana rekodi mbovu ugenini katika hatua hii kwani katika michezo yao sita ugenini katika hatua hii ya mtoano wamefanikiwa kushinda mchezo mmoja tu.

Manchester City wamewahi kupita katika hatua hii mara moja tu katika msimu wa 2015/2016 ambapo walikwenda hadi nusu fainali ambayo walipoteza baada ya kutolewa na mabingwa watetezi Real Madrid.

Mchezo huu unaweza kuwa vita kati ya washambuliaji wawili Dimitri Oberlin wa Fc Basel na Raheem Sterling wa Manchester City ambao wote wawili wamefunga mabao manne manne katika michezo mitano iliyopita ya Champions League.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here