Home Kitaifa TFF imetangaza kumfungia Juma Nyoso

TFF imetangaza kumfungia Juma Nyoso

6082
0
SHARE

Kamati ya nidhamu ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) imetangaza kumfungia  Juma Nyoso wa Kagera Sugar kwa kosa la kupiga shabiki baada ya mchezo kati ya timu yake dhidi ya Simba kwenye uwanja wa Kaitaba, Bukoba.

“Kamati ya nidhamu ya TFF ambayo pia ilijadili mambo mengine, ilijadili shauri ambalo lilifikishwa kwenye kamati hiyo ambalo lilimuhusu mchezaji wa Kagera Sugar Juma Nyoso kuhusiana na tukio lake ambalo lilitokea kwenye mchezo uliozikutanisha Kagera Sugar na Simba kwenye uwanja wa Kaitaba”-Clifford Ndimbo, afisa habari TFF.

“Juma Nyoso alituhumiwa kumpiga shabiki baada ya kumalika kwa mchezo kinyume na kanuni za ligi kuu zinazozungumzia mchezo wa kiungwana.”

“Kamati ilipitia ripoti ya kamishna wa mchezo ambayo imeeleza tukio la kupishana kwa Juma Nyoso na shabiki ambaye alikuwa amebeba vuvuzela na Juma Nyoso akaonekana kusimama na kuanza kumpiga shabiki yule kwa kutumia kiatu na baadaye akamuinamisha na kuanza kumpiga kwa kutumia goti.”

“Kamati ilimwita Nyoso kujitetea, kwa upande wake alikataa madai hayo ya kumpiga shabiki. Alisema alichofanya ilikuwa ni kumkunja tu shabiki huyo lakini hakumpiga.”

“Kamati imemtia hatiani Juma Nyoso kupitia kanuni za ligi kuu na katiba ya TFF lakini ilipokea taarifa za nyuma za Nyoso kwamba aliwahi kuadhibiwa kwa makosa ya utovu wa nidhamu. Kwa hiyo kamati imemfungia Nyoso mechi tano pamoja na faini ya shilingi 1,000,000 (milioni moja).”

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here