Home Kimataifa Rekodi hii ya penati inaonesha undugu kati ya Barcelona na marefa?

Rekodi hii ya penati inaonesha undugu kati ya Barcelona na marefa?

7813
0
SHARE

Kesho ni tarehe 14 mwezi February, ni tarehe ya wapendanao/valentine day. Lakini kwa Barcelona tarehe 14 February ina maana nyingine kabisa kwano ni siku wanayokumbuka mara ya mwisho kupigiwa penati.

Ilikuwa mwaka February 14 mwaka 2016 ndio ilikuwa mara ya mwisho kwa Barcelona kupigiwa penati na tangu kipindi hicho hadi hii leo hakuna refa aliyetoa penati kwa timu pinzani dhidi ya Barcelona.

Celta Vigo walikuwa timu ya mwisho kupewa penati mbele ya Barcelona japo katika mcgezo huo walipigwa kipigo cha mbwa mwizi cha mbao 6 kwa 1 na mchezaji wa mwisho kuwapigia Barcelona penati alikuwa ni John Guidetti.

Toka siku hiyo hadi hii leo katika La Liga kumeshatolewa penati 224 kwa timu nyingine lakini hakuna hata penati moja kati ya penati hizo ambayo imepigwa kuelekea katika lango la Barcelona.

Real Madrid wenyewe zimeshapigwa kuelekea lango lao lakini vinara wa kupigiwa penati ni Celta Vigo na Valencia ambao wote hadi sasa wamepigiwa jumla ya penati 18.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here