Home Kitaifa Mbabe wa Okwi aangukia kifungoni

Mbabe wa Okwi aangukia kifungoni

6329
0
SHARE

Kama unakumbuka Februari 4, 2018 mlinzi wa Ruvu Shooting Mau Bofu alimpiga kiwiko mshambuliaji wa Simba Emanuel Okwi muda mfupi kabla ya mapumziko na kumsababishia maumivu yaliyopelekea kushindwa kuendelea na mchezo huo.

Leo Februari 13, 2018 kamati ya saa 72 imetoa maamuzi mbalimbali ikiwa ni pamoja na kutolea maamuzi kuhusu tukio la Mau Bofu kumpiga Okwi.

Mau Bofu amefungiwa mechi tatu na kupigwa faini ya Tsh. 500,000 (laki tano) kwa kumpiga kiwiko Emmanuel Okwi katika mechi hiyo iliyofanyika Februari 4, 2018 kwenye uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam. Adhabu hiyo imezingatia Kanuni ya 37(3) ya Ligi Kuu kuhusu Udhibiti wa Wachezaji.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here