Home Kimataifa Maurcio Pochettino kuwatumia Juventus kuweka rekodi hii Champions League

Maurcio Pochettino kuwatumia Juventus kuweka rekodi hii Champions League

4838
0
SHARE

Champions League imerejea na hii leo 16 bora ya mashindano hayo inaanza, huu utakuwa mchezo wa kwanza kati ya Juventus na Tottenham Hotspur katika mashindano haya.

Kocha Maurcio Pochettino atakuwa katika nafasi ya kufanya jambo ambalo wenzake waloshindwa, nalo ni kwenda robo fainali kwani mara mbili ambazo Tot walifika katika hatua hii walishindwa kusonga mbele na kama akiipeleka Tot robo fainali atakuwa kocha wa kwanza kufanya hivyo.

Lakini Juventus ni kati ya timu ambazo hazina mchezo katika Champions League kwani michezo yao 19 iliyopita ya mashindano haya wamefungwa michezo miwili tu( fainali vs Real Madrid na mchezo wa makundi vs Barcelona).

Sii hivyo tu bali michezo 22 ambayo Juventus wamecheza katika uwanja wao wa nyumbani katika michuano hii ya Champions League hawajapoteza hata mchezo mmoja, mara ya mwisho walifungwa 2013 na Bayern Munich.

Lakini hii haiwapi kiburi Juventus mbele ya Tottenham Hotspur kwani Tottenham ni kati ya timu nne ambazo hazijapoteza mchezo hata mmoja katika Champions League msimu huu,nyingine ni Liverpool, Barcelona na Besitkas.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here