Home Kimataifa Manchester United wazidi kutamba kwa mauzo ya jezi

Manchester United wazidi kutamba kwa mauzo ya jezi

5937
0
SHARE

Wametoka kupigwa bao moja kwa nunge na Newcastle mwishoni mwa wiko lakini hii haijawagharimu Manchester United jambo lolote kibiashara kwani rekodi zinaonesha United wanaongoza kwa rekodi ya mauzo.

Katika orodha ya majina 20 ya wachezaji ambao jezi zao zinaongoza kwa kuuzwa kuanzia January 1 mwaka huu klabu ya Manchester United imefanikiwa kutoa jumla ya wachezaji 6 katika orodha hiyo.

Na bado mchezaji ambaye jezi yake imeuzwa zaidi katika kipindi hicho ni nyota wa Manchester United Alexis Sanchez na inaonesha tangu aende United ndio mwanasoka ambaye jezi yake imenunuliwa zaidi.

Anayemfuatia Alexis Sanchez katika orodha hiyo ni kiungo wa Manchester United Paul Pogba ambaye kabla ya Sanchez kwenda Manchester United alikuwa akiongoza orodha hiyo.

Harry Kane anashika nafasi ya tatu kisha Mohamed Salah anashika nafasi ya nne, Eden Hazard yuko nafasi ya tano na Phillipe Coutinho akishika nafasi ya sita, Kelvin De Bruyne nafasi ya saba huku Mesut Ozil akishika ya nane.

Roberto Firmino yuko nafasi ya tisa na ya kumi ni Zlatan Ibrahimovich, wachezaji wengine wa United walioko 20 bora ni Romelu Lukaku (13), David De Gea(14) na Marcus Rashford yuko katika nafasi ya 18.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here