Home Kimataifa Man City hawazuiliki, Tottenham nao waigomea Juve

Man City hawazuiliki, Tottenham nao waigomea Juve

5279
0
SHARE

Sergio Kun Aguero alifunga moja ya bao wakati City wakiifunga Fc Basel  bao 4 kwa nunge ,na sasa Aguero anakuwa mchezaji wa pili kufunga katika michezo minne ugenini katika Champions League kwa timu zinazotokea Uingereza baada ya Dwight Yorke.

Lakini pia assist ya Kelvin De Bruyne katika bao la kwanza la Ikay Gundogan inamfanya Mbelgiji huyo kufikisha jumla ya assist 19 katika mashindano yote ikiwa ni assists 5 kuliko mchezaji yeyote EPL.

Kwa sasa kikosi hicho cha Pep Gurdiola wanakuwa wameshinda mechi nyingi hadi sasa (34) ikiwa ni idadi kubwa ya ushindi kuliko waliopata msimu mzima uliopita (33).

Juventus nao kabla ya usiku wa leo walikuwa wamefunga mabao 3 tu kati ya 75 yaliyopita katika dakika 10 za mwanzo lakini mchezo wao vs Tottenham walifanikiwa kufunga mabao 2 ndani ya dakika 10 za mwanzo kupitia Gonzalo Higuain.

Tottenham walitokea nyuma kwa mabao mawili na kusawazisha kupitia Harry Kane na Christian Eriksen na sasa Harry Kane anakuwa mchezaji anayeongoza kwa mabao katika ligi kubwa 5 barani Ulaya (ana mabao 33).

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here