Home Kitaifa Ushindi finyu wa Yanga kimataifa, Shaffih Dauda ameona tatizo

Ushindi finyu wa Yanga kimataifa, Shaffih Dauda ameona tatizo

8451
0
SHARE

Weekend iliyopita vilabu viwili vya Tanzania (Yanga na Simba) vilicheza mechi zao za kwanza za mashindano ya kimataifa msimu huu vikiwa kwenye uwanja wa nyumbani.

Jumamosi Yanga walicheza mechi ya Caf Champions League na St Louis kutoka Seychelles na kufanikiwa kupata ushindi wa goli 1-0, Jumapili ilikuwa ni zamu ya Simba ambao walishinda 4-0 dhidi ya Gendarmerie ya Djibouti kwenye mchezo wa Caf Confederation Cup.

Ushindi wa Yanga nyumbani unaonekana ni finyu kuliko matarajio ya watu wengi ukilinganisha na aina ya mpinzani waliekutana nae (St Louis).

Shaffih Dauda anadhani ushindi huo mwembamba walioupata Yanga dhidi ya St Louis unatokana na wachezaji kukosa motisha na morali.

“Yanga kama wamekosa motisha, wanacheza kama hawako tayari lakini ratiba inawataka kufanya hiyo. Moja ya maeneo ambayo Yanga wanahitaji kufanyia kazi kwa sasa ni kujenga morali ya wachezaji”-Shaffih Dauda, mchambuzi wa michezo.

“Inaweza kuwaathiri kimbinu na kiufundi kama saikolojia ya wachezaji haijakaa vizuri kuweza kutekeleza majukumu kutoka kwenye benchi la ufundi.”

Ilikuwa imezoeleka vilabu vya Tanzania kupata ushindi mkubwa dhidi ya vilabu vinavyotoka mataifa ya visiwani kama Comoros na Seychelles.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here