Home Kimataifa UEFA yatoa darasa kuhusu kutamka majina ya nyota hawa katika Champions League

UEFA yatoa darasa kuhusu kutamka majina ya nyota hawa katika Champions League

12892
0
SHARE

Watoto wa mjini wanasema “Kinawaka”, hivyo ndivyo unavyoweza kusema ambapo Jumanne hii Champions League moto utawaka huku wafalme 16 waliobaki katika Champions League wataoneshana ubabe.

Lakini tatizo kubwa kwa mashabiki wengi wa soka dunia nzima ni jinsi ya kutamka majina ya wachezaji wengi nyota katika michuano hiyo suala ambalo kamati ya michuano hiyo imeamua kulitatua.

UEFA wameamua kutoa elimu juu ya utamkaji wa majina ya baadhi ya nyota wakubwa wa Champions League na hii inaonekana itawasaidia mashabiki wengi kufahamu jinsi ya kuwaita nyota wao.

Majina yaliyotolewa ufafanuzi ni ikiweml nyota wa Barcelona Lionel (Lee-oh-nell) Messi, Ivan Ractic (Ra-key-tich) na Thomas Varmaelen(Ver-mah-len).

Nyota wa Bayern Munich Roberto Lewandoski(Le-van-dov-ski), Manuel Neuer (Man-Well Noy-Er), James Rodriguez (Ha-mess Rod-ree-gess) na Joshua Kimmich(Kim-ikh).

Chelsea nao kuna Cesar Azpilicueta(Ath-pili-coo-et-ah), Gary Cahill(Kay-hill), Thibaut Courtois (Tib-oh Cort-wah),Olivier Giroud(Jee-roo) Eden Hazard(Ay-den),N’Golo Kante(Con-tay).

Liverpool kuna Emre Can(Jan), Simon Mignolet (See-mon Min-yo-lay), Georginio Wijnaldum(Why-nal-dum), Manchester City nako Kevin De Bruyne(De Bruh-nah), Ilkay Gundogan(Ilk-eye Gun-doe-wan), Gabriel Jesus (Jay-zooss) na Aymeric Laporte(Em-rick).

Manchester United nao kuna Davide De Gea(De Hayer), Victor Lindelof (Linda-love), Anthony Martial(Mar-see-al), Real Madrid ni Dani Carvajal(Car-va-hal), Dani Ceballos(Seb-eye-oss), Mateo Kovacic (Ko-va-chitch), Toni Kroos (Crows), Luka Modric(Mod-rich).

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here