Home Kitaifa Video-“Tulifikiri Simba wangetufunga 9 au 10”-kocha Gendarmerie

Video-“Tulifikiri Simba wangetufunga 9 au 10”-kocha Gendarmerie

6163
0
SHARE

Baada Gendarmerie kupoteza mchezo wao kwa magoli 4-0 dhidi ya Simba, kocha mkuu wa timu hiyo Mvuyekure Issa amesema mawazo na fikra zao kabla ya mchezo huo ilikuwa huenda wakafungwa magoli 9 au 10 lakini kutokana na namna walivyopambana wameweza kupunguza idadi ya magoli.

Kwa kifupi kocha huyo anamaanisha kufungwa 4-0 na Simba kwa upande wao wamefanikiwa kwa sababu idadi ya magoli waliyotarajia kufungwa ni tofauti na ilivyokuwa baada ya mchezo.

“Timu yangu ina vijana wengi chipukizi na nimeitayarisha kwa muda mfupi kwa ajili ya mashindano haya. Kwetu (Djibouti) tupo nafasi ya tatu kwenye ligi lakini msimu uliopita ndio tulikuwa mabingwa wa ligi tukapata nafasi ya kuwajilisha nchi kwenye mashindano haya”-Mvuyekure Issa kocha mkuu Gendarmerie.

“Nilifikiri Simba itatufunga magoli 9 au 10 ndiyo tulikuwa tumezoea hivyo, lakini sasa hivi magoli yanazidi kupungua yamefika hadi manne, nadhani mwakani tutakuwa pazuri zaidi.”

“Tulikuja kucheza huku lengo letu kubwa ni kuzjia ili tusifungwe magoli mengi kwa sababu tulikuwa tunasikia wachezaji wa Simba ni machachari sana lakini sikuona kama tulivyokuwa tunatarajia.”

“Naenda nyumbani kujiandaa vizuri, nimeona makosa nitayarekebisha, tutajitahidi na sisi tupate ushindi nyumbani. Kila kitu kinawezekana kwenye mpira, siwezi kusema Simba watanifunga nyumbani. Titajitahi tupate ushindi ili tuwape faraja wadjibouti.”

“Magoli matatu yalitokana na makosa ya golikipa kwa sababu ndio amerejea kutoka kwenye majeraha amefanya mazoezi kwa siku chache ndiomaana hakuwa vizuri. Huyo ndio golikipa wa timu ya taifa pia.”

“Simba ni timu nzuri ina uwezo wa pesa inaweza kununua wachezaji wazuri na makocha wazuri pia.”

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here