Home Kitaifa Simba yatengua kauli ya Mzee Mwinyi

Simba yatengua kauli ya Mzee Mwinyi

8543
0
SHARE

Rais mstaafu wa awamu ya pili ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Alhaj Ali Hassan Mwinyi alikuwa mgeni rasmi wa mchezo wa Caf Champions League kati ya Simba dhidi ya Gendarmerie ulioshuhudiwa Simba ikipata ushindi wa mabao 4-0.

Mzee Mwinyi alivutiwa na soka la Simba lililooneshwa kwenye mchezo huo na baada ya mechi alifuta kauli yake aliyoitoa miaka 30 iliyopita alipokuwa uwanja wa Mkwakwani Tanga kwamba kwenye soka “Tanzania ni kichwa cha mwendawazimu” .

“Nimeshuhudia mchezo mzuri na sasa nafuta lile neno kwamba Tanzania ni kichwa cha mwendawazimu kila anaetaka kujifunza kunyoa atunyoe sisi, sasa nyie ndio vinyozi.”

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here