Home Ligi EPL “Nimeinunia Manchester United”-Haji Manara

“Nimeinunia Manchester United”-Haji Manara

9684
0
SHARE

Nani asiyejua kama afisa habari wa Simba Haji Manara ni Manchester United lia-lia? Kama ulikuwa hujui basi chukua hiyo kwamba Manara ni shabiki wa kutupwa wa mashetani wekundu wa Old Trafford.

Sasa kutokana na mfumo wa kujihami ‘kupaki bus’ anaoutumia kocha Jose Mourinho, mfumo huo unamkera sana Manara kiasi cha kuamua kuinunia Manchester kwa kuacha kulipia king’amuzi chake cha DSTV kwa hiyo haangalii mechi za Man Utd.

“Mimi sio mpenzi wa soka la kujihami, Mourinho ananiudhi mimi nataka kuburudika sio kushinda tu, nataka kuona ‘sambusa’ kidogo au ‘kijiko’ ndiyomaana nimechagua kushabikia Simba.”

“Kwa namna Mourinho alivyo, sikumoja tutamuona Sanchez anacheza centre-half.”

“Nimeinunia Manchester siangalii mechi zao, sijalipia king’amuzi cha DSTV toka mwezi wa 11 mwaka uliopita kutokana na mfumo, tunapakije basi tuna mchezaji kama Sanchez, Martial na Mata?”

“Kwa aina ya wachezaji tulionao Manchester United tukimpata kocha kama Guardiola ingekuwa balaa lakini Mourinho kazi yake ni kuchukua treni ya TAZARA kuipaki nyuma utamfunga nani?”

Jana Februari 11, 2018 Mourinho aliendeleza rekodi yake ya kushindwa kupata ushindi kwnye uwanja wa St James Park kwa mechi za EPL baada ya Manchester United kuchezea kichapo cha bao 1-0 mbele ya Newcastle United.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here