Home Kitaifa Maxime bado hajakata tamaa na Kagera yake

Maxime bado hajakata tamaa na Kagera yake

4388
0
SHARE

Kocha wa Kagera Sugar Mecky Maxime amesema bado hajakata tamaa licha ya timu yake kuwa na mwendo wa kususua kwenye mechi za ligi kuu Tanzania bara huku akiamini timu yake itafanya vizuri.

Leo Februari 12, 2018 kikosi cha Maxime kimetoka sare ya kufungana 1-1 dhidi ya Azam kwenye uwanja wa Kaitaba, Bukoba na kupata pointi moja.

“Wote tuna macho tunaona mchezo, lakini haihusiani na matokeo, sisi kinachotuhukumu ni matokeo lakini bado sijakata tamaa bado nawapa moyo vijana wangu naamini tutafanya vizuri.”

“Mechi ilikuwa nzuri vijana wamepambana kadiri ya uwezo wao wamepata goli nao wamesawazisha mchezo umemalizika kwa sare tumepata pointi moja sio mbaya.”

Sare ya leo imeifanya Kagera Sugar kufikisha pointi 14 ikiwa katika nafasi ya 15 kwenye msimamo wa ligi. Azam imebaki katika nafasi ya tatu ikiwa na pointi 34 sawa na Yanga lakini tofauti ya magoli inazitofautisha timu hizo lakini Azam imeshacheza mechi 18 Yanga imecheza mechi 17.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here