Home Kimataifa Tangu Eden Hazard ajiunge EPL ndiye anaongoza kwa kwa kupigwa viatu Uingereza

Tangu Eden Hazard ajiunge EPL ndiye anaongoza kwa kwa kupigwa viatu Uingereza

6299
0
SHARE

Mwaka 2012 ndio mwaka ambao Eden Hazard aliamua kujiunga na ligi ya EPL akitokea Ligue One na tangu kufika Uingereza amekuwa kati ya washambuliaji bora sana na kiwango chake kimekuwa hivyo kwa muda.

Lakini mti wenye matunda ndio hupigwa mawe na hii ndio hali inayoendelea kwa Eden Hazard kwani tangu mwaka huo ambao alikuja EPL ukiachana na ubora wa Mbelgiji huyo lakini anaongoza kwa kupigwa viatu/faulu.

Hazard amechezewa rafu zaidi ya mara 500 katika ligi kuu ya Uingereza ikiwa ni zaidi ya mara kama 148 ambazo Raheem Sterling wa Man City amechezewa kwani rekodi zinaonesha Sterling amekwatuliwa mara 362.

Baada ya Eden Hazard na Raheem Sterling kunakuja raia wa Ivory Coast na klabu ya Crystal Palace Wilfred Zaha ambaye Zaha toka kipindi Hazard aje EPL naye pia amechezewa rafu mara 327.

Alexis Sanchez ambaye rekodi zinaonesha mechi mbili zilizopita EPL amekwatuliwa zaidi kufikia mchambuzi Jamie Carragher  kusema Sanchez hakwatuliwi kwa kuwa analipwa sana bali anakwatuliwa kwa kuwa ni bora, kwa ujumla Sanchez amepigwa kiatu mara 263.

Wakati Hazard anaongoza kwa rafu tangu mwaka 2012 lakini msimu wa 2017/2018 hayuko hata 3 ya juu ya waliochezewa rafu orodha inayoongozwa na Richarlison wa Watford(77) anafuatiwa na Dele Alli(66) kisha Jordan Ayew Swansea (62).

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here