Home Kimataifa Skendo “Nyota wa Newcastle aeleza alivyokoswakoswa kufanya mapenzi ya jinsia moja na...

Skendo “Nyota wa Newcastle aeleza alivyokoswakoswa kufanya mapenzi ya jinsia moja na mjomba wake”

9024
0
SHARE

Ama kweli duniani kuna mambo, hivyo ndivyo unavyoweza kuelezea mkasa huu wa nyota wa zamani wa Newcastle United ambaye amekaa na siri nzito katika kifua chake kwa muda wa miaka 28 sasa na hatimaye ameamua kuieleza dunia.

Ni Kieron Courtney Dyer kiungo wa zamani wa vilabu vya Newcastle, West Ham, QPR na Middlesbrough, Dyer kwa waliomuona wanasema alikuwa kati ya viungo mafia ambao walikuwa serious kazini.

Lakini kwa wakati wote Dyer anacheza soka hadi anastaafu alikuwa na tatizo kubwa na alibeba habari nzito moyoni mwake habari ambayo anaamini ilibadili kwa kiasi kikubwa sana maisha yake duniani.

Wakati wa utoto wake Dyer hakufanikiwa kuishi sana na mama yake kwani kazi ya mama yake ilikuwa ni usiku na hivyo ilimbidi akae na bibi yake ambaye nae aliachana na babu yake, Dyer aliishi na bibi huyo pamoja na ndugu yao aitwaye Kenny.

Siku moja usiku wakati Dyer akiwa sebleni akiangalia TV na uncle wake Kenny, kwa bahati mbaya Dyer alipitiwa na usingizi na kwakuwa alikuwa na mjomba wake huyo ilibidi alale katika mapaja yake kwani bado alikuwa mdogo.

Dyer anasema wakati ameshtuka usingizini alihisi kama ndugu yake huyo anachezesha sehemu zake za kiume jambo ambalo lilimshtua ila kwa kuwa ni ndugu yake aliogopa hata kupiga kelele wala kuamka.

Baada ya kubana kwa muda mrefu Dyer aliamka na akakuta Kenny(ndugu yake akimchezea sehemu zake za siri), Dyer alibaki akishangaa na ghafla ndugu yake alimvua suruali yake na kumuahidi wafanye atakacho atamnunulia chocolate.

Dyer anadai aliendelea tu kushangaa na ghafla akakuta ndugu yake ameshamvua suruali yote na ameinamisha kichwa kama anataka kufanya ngono kwa njia ya mdomo(oral sex) ndipo Dyer akafanikiwa kumsukuma na kuondoka.

Baada ya kufanikiwa kumsukuma, Dyer alikimbilia simu na kutaka kumpigia mama yake lakini ghafla Kenny alikuja kwa mbele na kumuonesha alama ya kukaa kimya na Dyer alishindwa kupiga simu akakaa kimya na hiyo ikawa siri yake.

Bahati mbaya wakati Dyer akiwa na miaka 21 Kenny alifariki dunia na Dyer anasema alipokwenda kwenye msiba wake alikuwa kijiuliza kwanini amlilie mtu mwenye tabia za kishetani kama Kenny.

Lakini kama hujui tu ni kwamba baada ya Dyer kusaini Newcastle alikuwa kati ya wanasoka wanaolipwa zaidi nchini Uingereza na pia alifanikiwa kuitumikia England kombe la dunia 2002 na michuano ya Euro 2004.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here