Home Kitaifa “Benchi lilianza kunipoteza Simba”-Jonas Mkude

“Benchi lilianza kunipoteza Simba”-Jonas Mkude

12078
0
SHARE

Kiungo wa Simba Jonas Mkude ambaye yuko moto kwa sasa amekiri kwamba huenda benchi lingempotezea ubora wake. Mkude hakuwa na nafasi ya kucheza mara mechi za kwanza msimu huu wakati Simba ilipokuwa chini ya kocha Joseph Omog ambaye baadaye alitimuliwa katika timu hiyo.

Mkude amesema tayari alishaanza kupoteza kujiamini kutokana na kuwekwa ‘mkekani’ jambo ambalo lilianza kuathiri kiwango chake kiuchezaji. Wakati kocha mkuu wa Simba akiwa Omog aliwatumia zaidi Mzamiru Yassin na James Kotei katika eneo la viungo wa kati.

“Kiwango changu kilikuwa chini kwa sababu nilikuwa sipati nafasi, sikucheza hata mechi moja katika mechi sita za kwanza za ligi msimu huu, nilianza kucheza mechi ya saba lakini nikicheza moja au mbili inayofuata napumzishwa benchi kwa hiyo mwisho wa siku nadhani kujiamini kwangu kulipungua lakini kwa sasa nashukuru nipo vizuri” Mkude.

Mkude ni mchezaji ambaye amedumu Simba kwa muda mrefu, alikuwepo kwenye kikosi kilichocheza klabu bingwa Afrika mwaka 2012, amezungumzia umuhimu kama mchezaji kushiriki mashindano hayo makubwa barani Afrika kwa kwa ngazi za vilabu.

“Ni fahari kwa kila mchezaji kucheza mashindano ya kimataifa kwa sababu ni muda mrefu timu ilikuwa haijashiriki mashindano hayo mimi mwenyewe nikiwepo na wachezaji wengine walikuja kuongezeka.”

Mimi nilicheza kidogo japo wakati huo ndiyo nilikuwa naanza kupata nafasi, baada ya kushinda ubingwa wetu wa mwisho wa ligi 2011/12 nilicheza hapa mechi na ES Setif nikacheza mechi nyingine Sudan na Al Ahly Shendi ambao walitutoa kwenye mashindano.”

“Ni kiu ya muda mrefu ya wanasimba kuiona timu yao ikicheza mashindano ya kimataifa kwa hiyo ni muhimu sana wakatupa support kubwa, nadhani wanauona mwendo wetu tulionao kwenye ligi sasa hatutaki uishie huko tutaenda nao hadi kwenye mechi zetu za kimataifa ili tujitangaze pia kama kuna nafasi ya kutoka basi baadhi ya wachezaji waende kucheza nje.”

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here