Home Kitaifa Yanga wameanza kwa ushindi kimataifa

Yanga wameanza kwa ushindi kimataifa

4694
0
SHARE

Yanga wameanza kwa ushindi wakiiwakilisha Tanzania kwenye ligi ya vilabu bingwa Afrika baada ya kushinda 1-0 dhidi ya St.Louis ambao ni mabingwa wa Ushelisheli.

Mchezo huo wa hatua ya awali umechezwa kwenye uwanja wa taifa Yanga wakiwa wenyeji, mabingwa hao wa Tanzania watajutia nafasi kadhaa walizoshindwa kuzitumia kufunga magoli na kujikuta wakipata ushindi mwembamba wakiwa nyumbani.

Dakika ya 25 kipindi cha kwanza mshambuliaji wa Yanga Obrey Chirwa alikosa mkwaju wa penati uliotokana na Hassani Kesi kuangushwa kwenye penalt box.

Goli pekee la Yanga limefungwa na kiungo mshambuliaji Juma Mahadhi ambaye aliingia kipindi cha pili kuchukua nafasi ya Ibrahim Ajib.

  • Ni ushindi wa kwanza kwa Yanga kwenye mashindano ya kimataifa msimu huu lakini ukiwa ni ushindi wao wa tano mfululizo katika mechi tano zilizopita.
  • Chirwa amekosa mkwaju wa tatu wa penati kati ya mitano aliyopiga ndani ya miezi miwili (Januari na Februari).
  • Pius Buswita, Raphael Daudi, Ibrahim Ajib na Ramadhani Kabwili, wamecheza kwa mara ya kwanza mashindano ya kimataifa kwa ngazi ya vilabu.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here