Home Kimataifa Tottenham vs Arsenal wanaturudisha nyuma hadi 1993 hii leo

Tottenham vs Arsenal wanaturudisha nyuma hadi 1993 hii leo

3949
0
SHARE

Mchezo unaosubiriwa na wengi hii leo ni kati ya Tottenham Hotspur vs Arsenal mchezo ambao kwa mara ya kwanza mchezo huu unapigwa uwanja wa Wembley tangu nusu fainali ya FA mwaka 1993.

Mara ya mwisho katika uwanja huu wa Wembley timu hizi mbili kukutana Arsenal walishinda bao 1 kwa 0 mbele ya Tottenham huku bao pekee la Arsenal likiwekwa kimiani na Tony Adams.

Arsenal wanaonekana watemi wa Tottenham kwani timu hizi mbili kwa ujumla zimeshakutana mara 194 katika mashindano yote huku Arsenal wakishinda mara 81 na Tottenham wakishinda mara 62.

Tottenham wanakwenda katika mchezo huu wakiwa hawajapoteza mchezo hata mmoja katika mechi zao 8 zilizopita lakini michezo yao 5 ya mwisho wamepata suluhu 3 katika ligi kuu ya EPL.

Rekodi sio nzuri sana kwa Arsenal kwani michezo 15 iliyopita ya EPL vs timu 5 za juu Arsenal hawajashinda hata mmoja katika michuano ya EPL na mara ya mwisho ilikuwa January 2015 vs Man City.

Mchezaji mpya wa Arsenal Pierre Aubameyang atakuwepo hii leo na Aubameyang ana rekodi nzuri sana mbele ya Tottenham kwani katika michezo minne ambayo amekutana na Arsenal amefanikiwa kuwafunga mara 4, moja katika Champions League na matatu katika Europa.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here