Home Kitaifa A-Z ya Okwi, sababu zilizomrudisha VPL kutoka Tunisia na Denmark, atakachofanya baada...

A-Z ya Okwi, sababu zilizomrudisha VPL kutoka Tunisia na Denmark, atakachofanya baada ya kustaafu soka

8023
0
SHARE

Kwa sasa Okwi ndiyo story ya town bila ubishi kama huamini hivyo pia sikulazimishi endelea kuamini vinginevyo, amefunga magoli 13 kwenye ligi baada ya mzunguko wa 17, yeye pamoja na Bocco kwa pamoja wamefunga magoli 22 magoli mengi zaidi ya klabu ya Azam ambayo imefunga magoli 19.

Wengi wengependa kufahamu mambo mengi kuhusu mchezaji huyu lakini kubwa ni kuhusu kushindwa kwake kufanya vizuri baada ya kupata nafasi Tunisia na Denmark lakini imekuwa tofauti na matarajio ya wengi leo hii Okwi amerejea simba kucheza VPL amefunguka kila kitu kilichotokea hadi kupelekea kurejea tena kwenye soka la Afrika Mashariki.

Okwi ameanza kwa kasi kubwa ya ufungaji akiwa ndio mchezaji anayeongoza kwa idadi kubwa ya magoli tangu kuanza kwa msimu huu, amsema kufanya kwake vizuri kunatokana na ubora pia wa kikosi cha Simba msimu huu.

“Mpaka sasa hivi mambo yanaenda vizuri kwangu na kwa klabu yangu ya Simba, tunaongoza ligi mimi nikiwa juu ya wafungaji ni jambo la kushukuru.”

“Wachezaji ambao nimekutana nao msimu huu wengi ni wazuri na wazoefu kitu ambacho kinapelekea tufanye vizuri kwa sababu tunapambana pamoja kama timu kuhakikisha tunapata ushindi na mimi naendelea kupata magoli.”

Kama ilivyo kwa wachezaji wengi duniani, Okwi huendelea kujiweka fiti hata akiwa kwenye mapumziko kitu ambacho kinamfanya awe wa moto anaporejea kwenye majukumu ya klabu yake.

“Mchezaji yeyote duniani akiwa mapumzikoni hawezi kukaa muda wote, mchezaji mpira kazi yake ni kucheza kwa hiyo lazima uwe tayari muda wote utakapohitajika kufanya kazi uwe tayari kwa hiyo lazima ufanye mazoezi ya kawaida kama kwenda gym na kufanya road work.”

Hakuna jambo lisilo na mwisho, itafika wakati okwi hatoweza tena kupambana na mabeki uwanjani akiachana na soka anataka kuwa wkala wa wachezaji.

“Baada ya kuacha mpira malengo yangu ni kuwa agent kwa sababu napenda sana wachezaji wa baade wafaidike sana na mpira ili wafurahie mpira na waweze kunufaika na vipaji vyao kwa hiyo nitapambana sana kuhakikisha wachezaji wa baadaye hawapati matatizo ambayo sisi tumepata. Wanatakiwa kupita kwenye njia nzuri ili wafanikiwe zaidi.”

Amefunga magoli 13 kwenye ligi, magoli yote akifunga kwenye viwanja viwili vya Dar (uwanja wa Uhuru na uwanja wa Taifa), mawali amablo wadau wengi wanajiuliza ni kwa nini ameshindwa kufunga viwanja vya mikoani?

“Hata nje ya Dar es Salaam napata nafasi lakini nakosa, hapa Dar napata nafasi nafunga kwa hiyo ni namna tu ya kutumia nafasi vizuri itafika wakati nitafunga lakini hadi sasa ni jambo la kushukuru mambo yanaenda vizuri kwa hiyo kufunga kwenye viwanja vya nje ya Dar ni jambo la kupambana na kuongeza juhudi magoli yatakuja popote kwa sababu ligi bado mbichi sana.”

Malengo yake ni kufikisha magoli mangapi msimu huu? Ukiachana na yeye kuwa na jina kubwa ndani ya klabu ya simba na soka la Tanzania, anachukia wachezaji wanaokamia wengine na wanadhani kuwazuia baadhi ya wachezaji ni lazima uwaumize.

“Kama mshambuliaji malengo yangu ni kuisaidia timu yangu kuhakikisha tunapata pointi tatu, kitu ambacho kinanikera ni watu ambao huwa wanapania wenzao bila kufikiria kwamba tunapokuwa uwanjani wote kazi yetu ni mpira, familia zetu zinatutegemea kwa sababu ya mpira na kipato tunachopata ni kutokana na mpira kwa hiyo unapokuwa na nia ya kumuumiza mwingine si jambo zuri.”

“Timu yetu ya Simba tunakamiwa sana, tunagongwa-gongwa sana lakini huwezi kuona wachezaji wa Simba wakiwachezea rafu za makusudi wachezaji wengine. Rafu nyingine ni za kimpira na zinatokea uwanjani lakini kuna baadhi ya timu zinafikiri kuizuia Simba lazima uwagonge na kuwaumiza wachezaji kitu ambacho waamuzi wanatakiwa kukiangalia sana.”

Mara kadhaa mashabiki wa Simba wamelalamikaia tabia ya Okwi kuchelewa kurudi kujiunga na timu yao pindi anaporudi kwao Uganda, ni kitu gani huwa kinasababisha kuchelewa kwake?

“Tatizo haliwezi kufanana siku zote, wakati mwingine inakuwa ni mambo ya kifamilia lakini kilchotokea hapa mwisho nilikuwa nasumbuliwa na nyonga kwa hiyo niliruhusiwa na timu na walikuwa wanafahamu nipo wapi kitu ambacho kilikuwa wazi na inapotokea suala la utovu wa nidhani ni klabu ndiyo inashughulika na jambo hilo lakini hakukuwa na tatizo lolote na klabu yangu ilikuwa inajua kila kitu.”

Okwi amesema kunatofauti kubwa kuanzia wachezaji hadi uongozi wa Simba ya sasa na ile ya miaka ya nyuma ambayo ilishiriki mashindano ya kimataifa mara ya mwisho.

“Tofauti zipo nyingi sana, ukiangalia wachezaji waliokuwepo wakati ule wengi walikuwa wazoefu tofauti na waliopo sasa ambao wengi ni wapya na vijana. Kuna tofauti pia ya uongozi kwa sasa Simba ipo katika wakati mzuri sana kuliko ilivyokuwa kipindi kile.”

Watu wengi wanatamani kujua kutoka kwake nini kilitokea akashindwa kutoboa alipojiunga na Etoile du Sahel ya Tunisia na Sonderjysk Elitesport ya Denmark wakati kutokana na uwezo wake wengi waliamini Tunisia na Denmark ilikuwa ni njia tu hivyo walitarajia kumuona kwenye vilabu vikubwa vya Ulaya.

“Ndiyo maana mwanzo kabisa nilisema nataka nikimaliza kucheza nataka kuwa agent kwa sababu ningependa sana vilabu vyetu vya Afrika Mashariki viwaandae wachezaji kwa ajili ya kuvuka level fulani, ukiangalia level ya mpira wa Tanzania na Tunisia au Denmark ni tofauti sana. Kuna sababu kadhaa ambazo zilinitoa Tunisia pia kuna sababu zilizonitoa Denmark.”

“Tunisia ilikuwa ni sababu za kiuchumi, Etoile du Sahel kipindi hicho haikuwa kwenye nafasi nzuri ya kulipa mishahara ya wachezaji, ukiangalia kulikuwa na wachezaji wengi ambao walikuwa na madai kwenye klabu na wengi waliondoka, mimi walishindwa kunilipa kwa zaidi ya miezi mitatu kwa hiyo tukavunja mkataba nikarudi Uganda baadae nikaja Yanga.”

“Wakati naenda Denmark tayari nilikuwa najitambua na niliamini nitafanya vizuri kwa sababu ilikuwa nafasi kubwa ya kucheza Ulaya lakini kwa bahati mbaya mambo hayakuwa kama nilivyopanga. Sikupata nafasi sana lakini ukiangalia katika mwaka mmoja na nusu sikucheza hata asilimia tano ya michezo klabu kwa hiyo tukakaa na uongozi wa timu tukafikia makubaliano kwamba hakuna faida kwa kila upande.”

“Mimi kama mchezaji haiwezekani niendelee kukaa kwa sababu sikuwa nafaidika kwa chochote nikapoteza nafasi hadi timu ya taifa na kupoteza kujiamini kwa upande wa klabu wakawa hawawezi kuendelea tena kunilipa mshahara.”

“Timu za taifa na vilabu zinatakiwa kuangalia soka kuanzia chini kabisa kwa ajili ya kuwaweka tayari wachezaji kucheza level nyingine. Kuwajenga kinidhamu, technical na tactics kwa sababu mpira wa Ulaya upo tactical sana tofauti na sisi huku lakini huku hatufuatilii sana nidhamu ya mchezo.”

“Nilipofika Denmark kocha alikuwa nanisisitiza sana nicheze namba tisa lakini ukiangalia umbo langu na wachezaji wa Denmark walivyo ni warefu sana na wananguvu halafu ni nchi ambayo system yao iko tactical sana kwa hiyo nikashindwa kuingia kwenye mfumo wa kocha na yeye hakuwa tayari kubadili mfumo kwa ajili ya mtu mmoja.”

“Ni lazima tuwaandae wachezaji wetu wa baadaye tuhakikishe wanafanikiwa zaidi yetu sisi.”

Jumapili ya Februari 11, 2018 Simba itacheza mchezo wake wa kwanza wa kimataifa baada ya kusubiri kwa kipindi kirefu, okwi anawaita mashabiki uwanja wa taifa na kuwaahidi kufanya kweli dhidi ya Gendarmerie Nationale ya Djibouti.

“Nawapongeza mashabiki wetu kwa kutupa ushirikiano mkubwa kwenye mechi za ligi, Jumapili ndio tunaanza mechi zetu za kimataifa baada ya kipindi kirefu kupita bila simba kushiriki mashindano ya kimataifa, tunawaomba waje kwa wingi kutupa support na sisi tutahakikisha tunafanya vizuri na kupata ushindi utakao tuweka kwenye nafasi nzuri kwenye mechi yetu ya marudiano Djibouti.”

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here