Home Kimataifa Xavi ataja wachezaji wawili watakaochukua nafasi ya Messi na CR7

Xavi ataja wachezaji wawili watakaochukua nafasi ya Messi na CR7

19224
0
SHARE

Tayari umri unamtupa mkono Cr7 na migui yake imeshaanza kuonekana kuchoka, wengi wanaamini muda wa Cristiano Ronaldo kuwa bora umekwisha na sasa ni wakati wa vijana wengine kuvaa viatu vyake.

Cristiano Ronaldo mwenyewe amekiri kwamba kwa sasa hawezi kufanya yale aliyoyafanya akiwa na miaka 20, kauli ambayo inaonesha hata yeye mwenyewe ameshaanza kukubali kwamba uwezo wake umekwisha.

Swali kubwa kwa mashabiki wa soka ni kwamba ni nani atachukua ufalme wa Cristiano Ronaldo na Lioneil Messi katika ufalme wa soka? Mchezaji wa zamani wa Barcelona Xavi Hernandez ana jibu la swali hilo.

Xavi anaamini kwa sasa kama mmoja kati ya Ronaldo na Messi ataondoka katika ufalme wake wa soka baasi moja kwa moja itakuwa nafasi ya mshambuliaji wa PSG Neymar kuchukua nafasi ya kuwa bora duniani.

Xavi hana mashaka kuhusu Neymar anaamini kabisa Ballon D’Or itakayofuata baada ya Ronaldo na Messi atakuwa Neymar, lakini je nani mwingine anaweza kupambana na Neymar katika tuzo hiyo?

Ukiacha Neymar, Xavi anaamini Kylian Mbappe yuko katika nafasi nzuri kushindana na Neymar kugombea tuzo hiyo na hii inamaanisha kuna uwezekano mkubwa PSG wakatoa washindani wawili wa Ballon D’Or siku za usoni.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here