Home Kimataifa Sanchez ahukumiwa jela miezi 16 baada ya kukwepa kodi

Sanchez ahukumiwa jela miezi 16 baada ya kukwepa kodi

10798
0
SHARE

Hukumu ya kesi iliyokuwa ikimkabili mshambuliaji mpya wa Manchester United Alexis Sanchez imetoka hii leo na mshambuliaji huyo kuhukumiwa miezi 16 jela.

Sanchez alikuwa akikabiliwa na kesi ya ukwepaji kodi wakati alipokuwa nchini Hispania na mamlaka za kodi nchini humo zinadai Alexis alikwepa takribani £900,000.

Lakini kwa sheria za nchini Hispania Alexis Sanchez hatakwenda jela kwa kuwa hukumu yake haizidi miaka miwili na pia hii ni mara ya kwanza kwake kupewa hukumu ya namna hiyo.

Lakini mshambuliaji huyo atalazimika kulipa faini ya kiasi cha £525,000 kutokana na kosa hilo ambalo alilifanya katika miaka yake mitatu aliyokuwa akiitumikia Barcelona.

Hukumu ya Sanchez inakuja katika kipindi ambacho bado mamlaka za mapato nchini Hispania zinafanga uchunguzi kuhusu kocha Jose Mourinho ambaye naye anatajwa kufanya kosa kama hilo.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here