Home Ligi EPL Real Madrid walivyoisaidia Man United kiuchumi na kumtoa kwa mkopo Di Stefano...

Real Madrid walivyoisaidia Man United kiuchumi na kumtoa kwa mkopo Di Stefano baada ya Ajali ya Munich

12469
0
SHARE

Ukiiondoa Barcelona, hakuna klabu nyingine ambayo ina upinzani na Real Madrid katika kila sekta ya soka la kisasa kama Manchester United, kutoka kwenye soka la uwanjani, biashara, utajiri, ufuasi wa mashabiki mpaka umaarufu miongoni mwa mashabiki wa soka.

Miaka ya hivi karibuni vilabu hivi viwili bado vimekuwa havina mahusiano mazuri hasa upande wa biashara: Nani anakumbuka maneno ya chuki ya Sir Alex Ferguson wakati Real Madrid walipotaka kumsaini Cristiano Ronaldo kwa mara ya kwanza – alisema Madrid ni kundi la kihuni, asingeweza kuwauzia mchezaji kundi hilo alilolipa jina la ‘virus’. Hata hivyo mwishoni Fergie aliwauzia Madrid Cristiano Ronaldo kwa £80m, – baadae Madrid wakarudi kumvuruga akili David De Gea lakini uhamisho ukashindikana kutokana na ubovu wa mashine ya Fax, msimu huu United walimhitaji Alvaro Morata lakini Madrid wakampandisha bei mpaka £70m lakini baadae wakawauzia Chelsea kwa £58m.

Mahusiano ya timu hizi mbili yamekuwa ya ‘kinafki’ kwa miaka hii, lakini timu hizi mbili zilikuwa na mahusiano ya kindugu miaka 50 iliyopita yaliyochagizwa na urafiki baina ya Rais wa klabu ya Real Madrid wa kati huo Santiago Bernabeu na Kocha wa Manchester United wa wakati huo Sir Matt Busy.

Urafiki wa Bernabeu na Busby ulikuwa mkubwa ambao ulipelekea ukaribu wa vilabu vyao, jambo lilopelekea Madrid kuisaidia United wakati ilipopata matatizo ya ajali ya ndege. Baada ya mchezo wa nusu fainali ya kombe la ulaya mnamo April 1958, ambapo Madrid kwa jumla ya magoli 5-3, mchezo wa kwanza Madrid walishinda 3-0 nyumbani, mchezo wa pili uliopigwa Old Trafford ukaisha kwa sare ya 2-2.

Santiago Bernabeu alivutiwa sana na hali ya kujituma ya vijana makinda wa United mpaka akafikia hatua ya kutaka kumpa ajira Sir Matt Busby. Hata hivyo kocha huyo mscotish alikuwa na hamu ya kushinda ubingwa wa ulaya na United hivyo akaikataa ofa ya Bernabeu kwenda kuifundisha Madrid.

Miezi 10 baadae, timu ya vijana makinda ya United ilipatwa na janga kubwa. Ajali ya ndege iliyotokea jijini Munich, miaka takribani 55 iliyopita, ajali ambayo ilichukua maisha ya vijana 8, wafanyakazi 3 na abiria wengine 10. Timu hiyo ilikuwa imetoka kushinda mchezo wa kombe la ulaya hatua ya robo fainali. Ndoto ya Matt Busby ya kuiteka ulaya na vijana wake wadogo ilionekana imefikia ukingoni

United wakaenda kupoteza mchezo wa nusu fainali vs Milan miezi 3 baadae baada ya ajali na AC Milan wakaenda kufungwa 3-2 na Real Madrid katika fainali. Rais Bernabeu akasema kwamba ushindi huo ni maalum kwa marafiki zake waliopotea kwenye ajali ya Manchester United na alifikia hatua ya kutoa ofa ya kuwapa United kombe, lakini United walikataa.

Kama hiyo haitoshi, Bernabeu akawashangaza wengi pale alipoamua kuwapa ofa ya usajili wa mkopo Manchester United ya mchezaji bora kabisa wa kipindi hicho barani ulaya Alfred Di Stefano kwa ajili ya msimu wa 1958-59. Bermabeu alienda kuongea na Di Stefano kuhusu uhamisho huo mkopo na mchezaji mwenyewe alikubali, sharti lilikuwa United wamlipe nusu ya mshahara wake na Madrid walikuwa walipe nusu nyingine mpaka mwishoni mwa msimu. Lakini tatizo likaja upande wa chama cha soka cha FA ambao waliuzuia huo kwasababu waliamini Di Stefano alikuwa anakuja kuchukua nafasi mchezaji wa kiingereza kwenye timu.

Baada ya msaada huo kushindikana, Madrid wakaamua kuisaidia United kwa njia nyingine. Wakatengeneza bendera maalum za kumbukumbu zilizokuwa na majina ya waliofarii kwenye ajali ya Munich, wakaiita jina la “Champions Of Honour”, bendera hii iliuzwa nchini Hispania ili kuisadia United kupata fedha. Pia kulikuwa na ofa ya majeruhi kwenda kutibiwa katika vitengo vya kisasa vya matibabu vya Madrid bila malipo yoyote.

Pia kulikuwa na michezo mingi ya kukusanya fedha baina ya timu hizi mbili. Ajali ya Munich iliiumiza United kiuchumi. Real Madrid kwa kipindi hicho walikuwa wakichaji kiasi cha £12,000 kwa ajili ya mechi za namna hiyo, lakini Bernabeu aliwaambia United ‘lipeni mnachoweza kulipa.’

Hii michezo haikuwa michezo ya kukusanya fedha tu. Kwa United kipindi hicho ndoto ya kuliteka soka la ulaya ilishakufa, kilichobaki sasa ilikuwa ni kujaribu kubaki ligi daraja la kwanza. Hivyo Matt Busby aliitumia michezo hii kuwajenga wachezaji wafikie level ya Puskas na Di Stefano na mashabiki pia walipaswa kusahau yaliyopita na kurudi kuisapoti timu vilivyo ikiwa walikuwa wanataka kurudi kucheza ulaya.

Mnamo October 1959 Madrid walishinda mchezo wa kwanza wa kirafiki kwa 6-1 mbele ya mashabiki 63,000 katika dimba la Old Trafford, huku Di Stefano, Puskas na Francisco Gento waking’ara.

Madrid wakashinda mchezo wa pili mwezi uliofuatia kwa 6-5, mchezo ambao ulitazamwa na mashabiki 80,000 ambao walikuwa wanazishangilia timu zote mbili.

Jioni yake siku hiyo Madrid wakaandaa shughuli ya kuchangisha fedha kwa ajili ya waliopoteza ndugu zao katika ajali ya Munich, Katika hafla hiyo alikaririwa akisema: ‘Busby sio mtu jasiri bali na kiongozi bora kabisa kuwahi kukutana nae kwenye soka duniani.”

Mchezo mwingine wa kirafiki uliofuatia, October 1960, Puskas na Di Stefano walikuwa majeruhi madogo. Bernabeu akamuuliza Busby kama alitaka mchezo upigwe kalenda lakini kocha huyo wa United akasisistiza kwamba Madrid sasa ni kama familia. Puskas na Di Stefano walivutiwa sana na tabia ya Busby na wakajilazimisha kucheza mechi hivyo hivyo na kuisaidia Madrid kushinda magoli 2-3.

United walianza kurudi kwenye ubora wao na katika mchezo uliofuatia wa kirafiki mnamo December 1961 waliwafunga Madrid 3-1, na mchezo uliofuatia pia wakashinda 2-0 mnamo September 1962. Baada ya hapo United wakashinda ubingwa wa kombe la FA msimu huo, kombe la kwanza kushinda baada ya ajali ya Munich, kombe hilo lilofuatiwa na kombe la ulaya mwaka 1968.

United waliwafunga Madrid katika nusu fainali kuelekea kwenda kushinda ubingwa wa ulaya na kutimiza ndoto ya Sir Matt Busby ambaye aliijenga United upya kwa miaka 10. Kocha huyo aliunda kikosi hatari kilichowamuisha mastaa wakubwa wa United kama Sir Bobby Charlton, Dennis Law na George Best.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here