Home Kimataifa Mchezaji “tapeli” wa Kiafrika alamba dili Liuthania kwa data za uongo

Mchezaji “tapeli” wa Kiafrika alamba dili Liuthania kwa data za uongo

8067
0
SHARE

Duniani kuna mambo, huko Lithuania mchezaji mmoja aliyetambulika kwa jina la Barkley Miguel Panzo ametumia taarifa za uongo mtandaoni ili kupata usajili kucheza nchini humo.

Taarifa zake katika mtandao wake wa Wikipedia zinadai kwamba yeye ni raia wa Angola ambaye ameshawahi kuitumikia timu yake ya taifa ya Angola katika michezo mitatu ya kimataifa.

Pia taarifa za Panzo zinaeleza kwamba ana miaka 25 tu na pia anadai kwamba aliwahi kuitumikia klabu ya QPR na kufunga jumla ya mabao 45 katika mechi 36 alizoichezea QPR.

Kwa taarifa hizo tu klabu moja ya nchini Lithuania iitwayo FK Panevezys haikusita kumuita Muangola huyo ili kumsajili na baada tu ya kusaini mkataba mwezi uliopita ndipo ukweli uliibuka.

Iligundulika kwamba Panzo kwanza hajawahi kuichezea Angola hata mechi moja na vile vile Panzo sio tu QPR bali hajawahi hata mara moja kucheza katika klabu yoyote nchini Uingereza.

Vilabu alivyochezea vingi vinaonekana ni vilabu vya chini nchini Ufaransa na Sweden na aliamua kutumia data za uongo katika Wikipedia ili asajiliwe timu kubwa, kwa sasa klabu iliyomsajili haina budi kuendelea kumlipa kwani tayari walishasaini mkataba.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here