Home Kitaifa Manara hataki Yanga wazomewe

Manara hataki Yanga wazomewe

5574
0
SHARE

Uongozi wa klabu ya Simba umewaomba mashabiki wake kutowazomea wachezaji wa Yanga watakapokuwa wanaiwakilisha Tanzania kwenye mechi ya kombe la vilabu bingwa Afrika Jumamosi dhidi ya St. Louis Suns United kwenye uwanja wa taifa.

Afisa habari wa Simba Haji Manara amesema, hawana undugu na Yanga lakini mashabiki wa Simba wasiwazomee kwa sababu watakuwa wanawakilisha nchi.

“Nawaomba mashabiki wa Simba wasiende kuizomea Yanga kwenye mechi yao ya kimataifa siku ya Jumamosi, kama hawawezi wasiende uwanjani. Sisi sote ni wawakilishi wa nchi, tunapofungwa na timu kutoka nje hawasemi wameifunga Yanga au Simba wanasema wameifunga Tanzania”-Haji Manara.

“Yanga si maadui zetu, ni watani zetu, ‘kucharurana’ kubaki kwenye mechi zetu za hapa nyumbani, kama wao watatuzomea ni wao siwezi kuwaomba wasifanye hivyo.”

Manara amesema Rais mstaafu wa awamu ya pili Alhaj Ally Hassani Mwinyi atakuwa mgeni rasmi kwenye mechi yao ya Caf Confederation Cup dhidi ya Gendarmerie Nationale siku ya Jumapili kwenye uwanja wa taifa.

Simba imetangaza viingolio kwa ajili ya mchezo huo ambapo kiingilio cha chini kabisa kitakuwa ni Tsh. 5000 kwa viti vya mzunguko.

Viingilio vingine katika mchezo huo ni VIP A Tsh. 30,000, VIP B Tsh. 20,000, viti vya Orange Tsh. 10,000.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here