Home Kitaifa Timu ya taifa ya Ghana imecheza VPL

Timu ya taifa ya Ghana imecheza VPL

7313
0
SHARE

Kama umeangalia kwa makini mchezo wa ligi kuu kati ya Simba vs Azam uliochezwa Februari 7, 2018 huenda utakuwa umegundua kwamba katika mchezo huo kulikuwa na kikosi cha wachezaji wa Ghana.

Jumla ya wachezaji nane (8) raia wa Ghana walicheza mchezo huo, idadi kubwa ya wachezaji wa kigeni kuheza kwa pamoja kaika mchezo mmoja.

Mchezo huo ambao ulimalizika kwa Simba kushinda 1-0 dhidi ya Azam, waghana sita walianza kwenye vikosi vya kwanza vya timu hizo. James Kotei na Asante Kwasi walianza kikosi cha kwanza cha Simba huku Razak Abarola, Daniel Amoa, Yakubu Mohamed na Enock Atta-Agyei walikuwa kwenye timu iliyoanza kwa upande wa Azam.

Baadaye Azam walifanya mabadiliko kwa kumuingiza Bernard Arthur (raia wa Ghana) kuhukua nafasi ya Yahya Zayd na Simba walimtoa Emanuel Okwi nafasi yake ikachukuliwa na Nicholas Gyan (raia wa Ghana)  ambao walikamilisha idadi ya waghana nane kucheza mechi hiyo.

Kwa sheria na kanuni za soka, zinaruhusu timu kucheza mechi ikiwa na wachezaji wasiopungua saba (idadi ya chini kabisa) lakini pia wasizidi 11 (idadi ya juu zaidi), kwa maana hiyo raia hao wa Ghana wangeunda kikosi chao cha wachezaji nane.

Kikosi cha wacheza wa Ghana waliocheza Simba vs Azam: Razak Abarola, Daniel Amoa, Yakubu Mohamed, Asante Kwasi, James Kotei, Nicholas Gyan, Enock Atta-Agyei, Bernard Arthur. (3-3-1).

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here