Home Kitaifa Baada ya kupanda ligi kuu, KCM inarudishwa kwa wananchi Kinondoni

Baada ya kupanda ligi kuu, KCM inarudishwa kwa wananchi Kinondoni

3695
0
SHARE

Baada ya kupanda daraja wiki moja iliyopita, timu ya KMC FC inayomilikiwa na Manispaa ya Kinondoni itatambulishwa rasmi kwa wanachi wa wila hiyo na mkoa wa Dar es Salaam kwa ujumla siku ya Jumamosi kwenye viwanja wa Biafra.

Mstahiki Meya wa Manispaa ya Kinondoni Benjamini Sitta amesema timu hiyo itapita mitaa mbalimbali ya wilaya ya Kinondoni kabla ya kufika uwanjani kwa ajili ya kuitambulisha.

“Timu hii inapanda kwa mara ya kwanza ligi kuu Tanzania bara lakini ukiondoa vilabu vikubwa vya Simba na Yanga, timu hii ikiwa ni mali ya umma kwa maana taasisi ya kiserikali imeweka historia ya kuigwa sisi tungependa iwe mfano kwa taasisi nyingine kuinua vipaji lakini kupendezesha huu mchezo tunaoupenda katika jamii zetu”- Benjamini Sitta.

“Kwa hiyo tumeamua siku ya Jumamosi iwe siku ya kuipokea timu katika viwanja vya Biafra, saa sita timu itgaondoka ofisi za Manispaa ya Kinondoni na kupita mitaa mbalimbali halafu saa nane itakuwa uwanja wa Biafra ambapo tungependa kujumuika na wana Kinondoni wote lakini wana Dar es Salaam wote. Atakuwepo mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, mkuu wa wila ya Kinondoni na viongozi mbalimbali.”

“Kutakuwa na burudani kutoka kwa wasanii wa muziki wa kizazi kipya kama Stamina, Roma, Madee na wasanii wengine wa Kisengeli ambao watahakikisha shughuli inapendeza. Tunafanya yote haya kwa ajili ya kuipongeza timu yetu.”

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here