Home Ligi EPL Vinara wanaofukuzia nafasi ya Antonio Conte hawa hapa

Vinara wanaofukuzia nafasi ya Antonio Conte hawa hapa

7360
0
SHARE

Kipigo cha bao 4 kwa 1 kutoka kwa Chelsea hakika kimewaweka Chelsea katika wakati mgumu haswa kocha wao Antonio Conte, kama Conte ataondolewa Chelsea wapo baadhi ya makocha ambao wanapewa nafasi kubwa kumrithi.

Luis Enrique. Kocha wa zamani wa Barcelona na ana rekodi ya kushinda Champions League lakini mwaka 2017 alitangaza kupumzika masuala ya soka lakini ni wazi kwa sasa anaweza kurudi kama Chelsea wakihitaji kufanga hivyo.

Diego Simeone. Kati ya vitu mashabiki wa Chelsea wanaweza kumiss kwa Antonio Conte ni mizuka yake katika eneo lake uwanjani, lakini Simeone naye ana tabia za Conte, iko wazi kwamba Simeone ana njaa na Champions League na kupata nafasi Chelsea ni muhimu kwake.

Massimiliano Allegri. Mwaka 2014 Allegri ndio alirithi mikoba ya Antonio Conte katika klabu ya Juventus lakini hata kabla ya Conte kujiunga na Chelsea tayari Allegri alianza kuhusishwa na Chelsea na sasa inaonekana Allegri anaweza tena kumrithi Conte.

Guus Hiddink. Hiddink ameshawahi kuwa kocha wa muda wa Chelsea lakini sasa ni kati ya makocha ambao wanatajwa sana kurudi Chelsea, aliwapa Chelsea FA mwaka 2009 na 2015 tena alirudi Chelsea na mwaka huu anaweza kurejea tena.

Maurzio Sarri. Kocha wa klabu ya Napoli, kwa sasa ni kati ga makocha ambao wanakubalika sana duniani kutokana na aina ya mpira ambayo Napoli wanacheza kiasi cha kumpelekea kocha wa Man City Pep Gurdiola kukiri kwamba Napoli ni timu bora zaidi aliyowahi kabiliana nayo msimu huu.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here