Home Kitaifa Okwi ameiteka Dar

Okwi ameiteka Dar

9154
0
SHARE

Mshambuliaji wa Simba Emanuel Okwi ameendelea kutesa kwenye viwanja viwili vya Dar es Salaam katika michezo ya ligi kuu Tanzania bara baada ya kuisaidia klabu yake kupata ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Azam.

Okwi alifunga bao hilo dakika ya 36 kwa kuunganisha krosi ya Asante Kwasi.

Mshambuliaji huyo raia wa Uganda amefikisha jumla ya mabao 13 kwenye ligi, jambo zuri au la kushangaza kuhusu Okwi ni kwamba magoli yake yote ameyafunga kwenye viwanja vya Dar (Uwanja wa Uhuru na Uwanja wa taifa).

Amefunga magoli nane (8) kwenye uwanja wa Uhuru huku magoli matano akifungia uwanja wa taifa. Hajafunga goli hata moja kwenye viwanja vya nje ya Dar katika mechi ambazo amecheza mikoani.

Mechi ambazo Okwi amefunga hadi sasa kwenye ligi kuu Tanzania bara

 • Simba 7-0 Ruvu Shooting (Okwi alifunga magoli manne, akawa mchezaji wa kwanza kufunga hat-trick msimu huu -Uwanja wa Uhuru.)
 • Simba 3-0 Mwadui (alifunga magoli mawili na kufikisha magoli sita -Uwanja wa Uhuru)
 • Simba 1-1 Mtibwa Sugar (akaendeleza rekodi ya kufunga mfululizo kwenye uwanja wa Uhuru na kufikisha magoli saba yote akiyafunga uwanja huohuo -Uwanja wa Uhuru.)
 • Simba 4-0 Njombe Mji (Okwi alifunga goli (1) la kwanza katika mchezo huo-Uwanja wa Uhuru)
 • Simba 4-0 Singida United (Okwi alifunga magoli mawili-Uwanja wa taifa)
 • Simba 4-0 Majimaji (Okwi alifunga magoli mawili-Uwanja wa taifa)
 • Simba 1-0 Azam (Okwi amefunga bao pekee katika mchezo huo-Uwanja wa taifa).

Okwi anafuatiwa kwa karibu na Obrey Chirwa wa Yanga katika orodha ya wachezaji waliofunga magoli mengi, Chirwa amefunga magoli 10 hadi sasa.

Ushindi wa Simba unaifanya ifikishe pointi 41 na kuendelea kubaki kwenye nafasi ya kwanza kwenye msimamo wa ligi, Yanga imebaki nafasi ya pili ikiwa na pointi 34, Azam ipo nafasi ya tatu ikiwa na pointi 33 wakati Singida United yenyewe ikiwa nafasi ya nne ikiwa na pointi 33 wakitofautishwa kwa wastani wa magoli na Azam.

Matokeo ya mechi zote za VPL zilizochezwa leo Februari 7, 2018

 • Simba 1-0 Azam
 • Mbao 1-2 Singida United
 • Ndanda 2-2 Mbeya City
 • Mwadui 3-1 Mtibwa Sugar
 • Majimaji 0-0 Tanzania Prisons
 • Stand United 0-0 Lipuli

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here