Home Dauda TV Video-Golikipa ‘kinda’ amezungumzia dakika zake 90 za kwanza VPL

Video-Golikipa ‘kinda’ amezungumzia dakika zake 90 za kwanza VPL

4994
0
SHARE

Golikipa kijana wa Yanga Ramadhani kabwili amedaka kwa mara ya kwanza kwa dakika zote 90 za mchezo wa ligi kuu dhidi ya Njombe Mji, hii ni mara ya pili kabwili anasimama golini kuidakia Yanga, mara ya kwanza ilikuwa kwenye mchezo dhidi ya Lipuli alipoingia kuchukua nafasi ya golikipa namba moja Youthe Rostand aliyeumia na kushindwa kuendelea na mchezo.

Katika dakika zote ambazo kabwili ameidakia yanga hajaruhusu goli, utakumbuka kuwa golikipa huyo ndiye alikuwa namba moja kwenye kikosi cha Serengeti Boys kilichoshiriki mashindano ya AFCON 2017 kwa vijana chini ya miaka 17.

Kabwili amesema anahitaji kucheza mechi nyingi mara kwa mara ili kuendelea kuimarisha kiwango chake na baadaye kuwa golikipa namba moja wa yanga: “Naamini nikipata nafasi zaidi ya hapa nahitaji kuonesha uwezo zaidi ili kuweza kujihakikishia nafasi.”

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here