Home Dauda TV Video-Baada ya kuifunga Azam “Sikusujudu, nilibusu uwanja”-Gadiel

Video-Baada ya kuifunga Azam “Sikusujudu, nilibusu uwanja”-Gadiel

5829
0
SHARE

Januari 27, 2018 Yanga ilikuwa ugenini kucheza dhidi ya Azam FC kwenye uwanja wa Azam Complex uliopo maeneo ya Chamazi nje kidogo ya jiji la Dar. Katika mchezo huo, beki wa kushoto wa yanga Gadiel Michael alikuwa anakutana kwa mara ya kwanza na timu yake ya zamani tangu asajiliwe na Yanga wakati wa dirisha la usajili kabla ya kuanza msimu huu (2017/18)

Gadiel amekulia katika kikosi cha vijana cha Azam kabla ya kupandishwa timu ya wakubwa na baadae kuwa mchezaji muhimu wa kokosi cha kwanza cha Azam, kijana huyo alifunga goli zuri lililoihakikishia Yanga ushindi wa 2-1 sasa gumzo likawa ni aina yake ya ushangiliaji baada ya kuifungia timu yake bao la pili huku akiwa ameifunga timu iliyomlea.

Dauda TV imepiga story na gadiel ambaye ameeleza kila kitu kuhusu alichomaanisha kutokana na style yake ya kushangilia lakini miongoni mwa alivyovisema ni kwamba hakusujudu bali alibusu uwanja, sasa kwanini aliubusu uwanja wa Azam Complex angalia vieo kupata majibu yote.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here