Home Ligi EPL Pogba na mbinu mbovu za Mourinho zilivyoisadia Spurs

Pogba na mbinu mbovu za Mourinho zilivyoisadia Spurs

17032
0
SHARE

Manchester United wana tatizo juu ya Paul Pogba. Ni mchezaji muhimu ambaye bila uwepo wake ni shida, lakini pia anayefanya maisha kuwa magumu kwa kwa kikosi cha Jose Mourinho pindi anapopewa majukumu ambayo hana uwezo nayo.

Na kuthibitisha hilo katika mchezo dhidi ya Tottenham Hotspur katika dimba la Wembley juzi Jumatano, Pogba alionyesha kiwango kidhaifu zaidi tangu ajiunge na United, na baada ya dakika 62 alitolewa nje na kocha wake Jose Mourinho. Timu yake ikiwa nyuma kwa magoli 2-0 na bado wakiwa wanapigiwa mpira mwingi na Spurs, ambao wachezaji wake 11 walikuwa na majukumu ambayo waliyamudu kulingana na uwezo wao, jambo lilopelekea kucheza vizuri zaidi ya wapinzani wao.

Turudi kwa Pogba, kiungo mwenye thamani ya £89m anayeifanya United icheze vyema sana …. anapopangwa mahala ambapo kunaendana na uwezo wa kipaji chake. Pale Wembley, alikuwa akicheza kwenye safu ya viungo wawili – akicheza pembeni ya Nemanja Matic – lakini, akiwa na miaka 24 hivi sasa, Pogba bado hajawiva kwenye kuwa na nidhamu kwenye ulinzi ili kuweza kucheza kwenye nafasi hiyo vizuri. Hivyo pindi anapochezeshwa kwenye mfumo wa viungo wawili anakuwa tatizo hasa pindi timu yake inapocheza dhidi ya timu bora.

Matamanio yake ya kwenda kucheza mbele zaidi hayaepukiki na mara zote amekuwa akipanda mbele na kumuacha Matic pekee yake na walinzi wakiwa hawana ulinzi wa kutosha, na hili lilionekana dhidi ya safu kali ya ushambuliaji ya Spurs, ambao waliishinda mechi ndani ya nusu saa tu ya mchezo.

Kama kiungo wa kati wa hadhi ya Pogba – anatakiwa kuwa na uwezo wa kuwa na umakini mkubwa ili kuweza kucheza kwa jukumu la kuzuia endapo atatakiwa kufanya hivyo kutokana na mazingira. Lakini hawezi kufanya hivyo, hilo limeshaonekana na sasa ni wazi ni ubishi wa Mourinho kubadili mbinu na sio kumtuma mchezaji wake staa kufanya kazi ya kuzuia mashambulizi dhidi ya wachezaji aina ya akina Dele Alli na Christian Eriksen.

Baada ya kuona Pogba akishindwa kutimiza maagizo aliyompa pamoja na kujaribu mara kadhaa kwa zaidi ya saa 1 ya mchezo – Mourinho aliamua kumtoa Pogba na kumuingiza Fellaini.

Chini ya Mourinho, baadhi ya wachezaji wamekuwa wakipewa ulinzi kuliko wengine – mmoja wao ni Pogba, lakini jana hali ilikuwa tofauti. .

Kutolewa katika mchezo dhidi ya Spurs baada ya kucheza kwa dakika 60, muda mfupi baada ya kuonekana akisemeshana kwa nguvu na Mourinho katika kipindi cha kwanza – kwa Pogba hili jambo zuri. Tangu aliporejea United akitokea Juventus, jana ilikuwa mara yake ya 4 kushindwa kumaliza mechi ya Premier League ambayo alianza.

Mchezo wa kwanza ulikuwa dhidi ya Crystal Palace mwezi May 2017, hapa Mourinho alimtoa kwa ajili ya kumuandaa na mchezo wa fainali ya Europa League vs Ajax, pia mnamo November 2017, akiwa ametoka kwenye majeruhi Pogba alicheza kwa dakika 70 tu, pia mchezo mwingine ambao hakumaliza ni ule aliopewa kadi nyekundu vs Arsenal.

Lakini safari hii vs Spurs, Pogba alitolewa kwenye mchezo kwasababu za kiufundi kama Mourinho alivyoeleza – kwamba alimuondoa kwa kuwa hakuwa anacheza vizuri. Hata hivyo Mourinho pia hawezi kuepuka lawama.

Kama Mourinho angempanga Ander Herrera pembeni ya Matic na kumtumia Pogba kucheza mbele yao, kama ilivyokuwa katika mchezo vs Everton mwezi uliopita wakati Pogba alipocheza kwa kiwango cha juu na kufanikiwa kuwa Man Of The Match – basi kiungo huyo mfaransa asingechexa vibaya vs Spurs kwa sababu angecheza eneo analolimudu zaidi kwa ufanisi mkubwa.

Lakini usajili wa Alexis Sanchez, ambaye ameiongezea makali safu ya ushambuliaji ya United, lakini pia ameleta mkanganyiko wa mbinu na majaribio ya kulitatua tatizo hilo lilifeli vibaya vs Spurs.

Wakati Pogba akicheza chini, Mourinho alimtumia Sanchez, Martial na Jesse Lingard nyuma ya mshambuliaji wa kati.

Martial na Lingard wameonyesha kwanini wanastahili nafasi katika kikosi cha kwanza hasa katika mechi za hivi karibuni, wakati Sanchez ilikuwa lazima aanze lakini watatu hao hawawezi kucheza nyuma ya mshambuliaji.

Kwanza kwasababu inamuondoa Pogba katika kucheza kwenye nafasi anayoimudu zaidi – nafasi ambayo anakuwa hatari zaidi kwa timu pinzani lakini pia inapelekea Mourinho kumpa majukumu mengine ambayo hayaendani na uwezo wake. Pogba sio mzuri kwenye kufanya ‘tackling’, sio mzuri kwenye kuzuia mipira ya juu na pia hana uwezo mkubwa wa kugundua hatari mapema kama ilivyo kwa viungo wa ulinzi. Pia anakosa nidhamu ya kubaki nyuma.

Kama au endapo Mourinho atafanya usajili wa kiungo mrithi wa Michael Carrick ambaye atacheza pamoja na Matic, Pogba atakuwa huru kucheza kwenye kiungo cha kushoto mbele – sehemu ambayo anaimudu vilivyo. Akileta madhara kwa timu pinzani na uwezo wake wa kuichezesha timu – akiwa kiunganishi cha nafasi ya ulinzi na ushambuliaji huku akitengeneza nafasi kwa washambuliaji.

Yote kwa yote, mchezo wa Spurs ulikuwa ukumbusho mwingine kwamba Pogba sio kiungo mkabaji na Mourinho alifanya makosa kumchezesha kwenye ulinzi vs Spurs.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here