Home Kitaifa Ni kiama ligi daraja la kwanza

Ni kiama ligi daraja la kwanza

6310
0
SHARE

Ligi daraja la kwanza ipo katika hatua za lala salama leo Ijumaa Februari 2, 2018 zinaweza kupatikana timu nyingine mbili kutoka Kundi B ambazo zitapanda kucheza ligi kuu msimu ujao zikiungana na JKT Tanzania ambayo yenyewe imeshapanda daraja kucheza ligi kuu msimu ujao ikitokea Kundi A.

Kutoka kundi b leo kutakuwa na vita kubwa kwa sababu mechi za kundi hilo zinahitimishwa leo ambapo timu mbili lazima zipande daraja kwa ajili ya kucheza ligi kuu msimu ujao, mechi zinazochezwa leo ni Mawenzi Market vs Coastal Union, Mufindi United vs Polisi Tanzania, Mbeya Kwanza vs Polisi Dar, na JKT Mlale vs KMC.

Mchezo kati ya JKT Mlale vs KMC utakuwa ukifuatiliwa na watu wengi kwa sababu timu zote zinakutana zikiwa zinalingana kwa idadi ya pointi (pointi 25) lakini JKT Mlale inaongoza kundi kutokana na wastani wao mzuri wa magoli.

Kocha wa kmc Fred Felix Minziro mechi hiyo ni fainali kwa sababu kila timu inanafasi ya kupanda kucheza ligi kuu msimu ujao

“Vita ni kubwa kwa maana ya kwamba JKT Mlale wanatafuta nafasi na sisi tunatafuta nafasi, vita itakuwa kubwa ukizingatia sisi tuliwatoa kwenye mchezo wa FA Cup kwa hiyo tunataka kuendelea kudhihirisha sisi ni timu bora. Mechi ya leo ni fainali tutaingia kushambulia moja kwa moja”, Minziro.

Balaa jingine litakuwa pale mkoani Morogoro kwenye uwnjan wa Jamhuri ambapo mechi kati ya Mawenzi Market vs Coastal Union itakuwa ikipigwa, Coastal Union inanafasi ya kupanda kucheza ligi kuu msimu ujao endapo itashinda mechi yake halafu JKT Mlale vs KMC zikatoka sare au timu moja ikashinda ntingine ikapoteza.

Wakati Coastal Union ikipambana kupanda daraja, Mawenzi Market yenyewe haina cha kupoteza kwa sababu ina point nane juu ya Polisi Dar ambayo inapointi tano, ili Mawenzi Market ishuke daraja inabidi Poilisi Dar ishinde idadi kubwa ya magoli dhidi ya Mbeya Kwanza ili iwe sawa pointi na Mawenzi Market halafu wastani wa magoli ndio uamue timu gani ya kushuka daraja na ipi itaendelea kubaki ligi daraja la kwanza.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here