Home Kimataifa Bao la Christian Eriksen sio la mapema zaidi EPL wala Tottenham, 10...

Bao la Christian Eriksen sio la mapema zaidi EPL wala Tottenham, 10 bora hii hapa

6096
0
SHARE

Sekunde 11 tu zilitosha Tottenham kuandika bao la kwanza dhidi ya Manchester United hapo jana lakini kama ulikuwa hujui, bao la Eriksen hapo jana sio bao la mapema zaidi katika ligi kuu nchini Uingereza, angalia 10 bora.

10.Peter Crouch. December mwaka 2014 wakati Stoke City wakiifunga Arsenal bao 3 kwa 2 moja kati ya mabao hayo yalifungwa na Crouch ambaye alitumia sekunde 19.

9.Jesus Navas. Manchester City waliidondoshea kipigo cha mbwa mwizi Tottenham kwa kuwapiga bao 6 kwa nunge mwaka 2014 lakini Jesus Navas aliwafunga Tot bao la mapema sekunde ya 13.

8.Jay Rodriguez. Ilikuwa Chelsea vs Southampton Jumapili ya tarehe 1 December 2013 na Rodriguez alitumia sekunde 13 naye kufunga bao hilo.

7.Asmir Begovic. Hii ni ya kuvutia zaidi kwani Begovic ndio golikipa pekee kuwahi kufunga bao la mapema katika historia ya EPL alitumia sekunde 13 na ilikuwa mechi kati ya Stoke City na Southampton.

6.Chris Sutton. Blackburn walikuwa ugenini kuwafuata Everton na aiku hiyo Sutton alifunga moja kati ya mabao mawili ya Blackburn Rovers akitumia sekunde 13.

5.Dwight Yorke. Yorke naye ilikuwa ni sekunde 13 lakini hii ilikuwa mwaka 1995 hapo kabla hajahamia United na aliifungia Aston Villa bao hilo wakati wakiiua Coventry bao 3 kwa 0.

4.Mark Viduka.Viduka sasa ni kama Eriksen tu kwani mwaka 2001 katika mchezo kati ya Leeds na Charlton na Mark Viduka naye alitumia sekunde 11 kufunga goli.

3.Christian Eriksen. Sasa Eriksen anatokea katika nafasi ya tatu kutokana na bao lake la usiku wa jana dhidi ya Manchester United ambapo alitumia sekunde 11 tu.

2.Alan Shearer.Newcastle wakiichapa Man City bao 2 kwa 0 mwaka 2003 na bao la kwanza la Newcastle lilifungwa na Shearer ambaye alitumia sekunde 10 tu.

1.Ledley King. Bao la Eriksen sio la mapema EPL bali pia sio bao la mapema Tottenham, Ledley King anashikilia rekodi ya bao la mapema zaidi EPL akitumia sekunde 10 mwaka 2000 wakati Tottenham wakienda sare ya bao 3 kwa 3 na Bradford.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here