Home Kitaifa Motisun yaingia kudhamini kriketi

Motisun yaingia kudhamini kriketi

2114
0
SHARE

Katika kuonesha kwamba sekta ya michezo nchini inakua na kupiga hatua mbele, kampuni ya Motisun Group  kesho januari 28, 2018 itazindua mashindano kriketi kwenye uwanja wa kawe huku timu sita zikianza kuchuana katika mchezo huo.

Meneja masoko wa kampuni hiyo Erhard Mlyansi amesema  lengo la kampuni yao kuingia kwenye mchezo wa kriketi ni kuongeza wigo wa tasnia ya michezo nchini na kuachana na dhana kwamba soka ndio linabeba taswira nzima ya michezo kwa sababu ya kuidhamini klabu ya Ndanda FC ya Mtwara inayoshiriki ligi kuu hivyo wameamua kutaza pia katika michezo mingine.

Erhard Mlyansi Meneja Masoko na Maendeleo Group

“Tumeamua kuongeza na kukuza sekta ya michezo nchini kwa kuingia pia kwenye mchezo wa kriketi ambao kwa hapa tanzania bado haujapata umaarufu mkubwa, ili nchi ifahamike kimichezo kimataifa ni vyema ikajihusisha na kufanya vizuri katika michezo mbalimbali ikiwemo kriketi”-Mlyansi, Meneja Masoko na Maendeleo Group.

“Kuingia kwetu kwenye kriketi haimaanishi tutaacha kusapoti soka, kwa upande wa soka tulianza na ndanda lakini huko mbele tutaangalia tuweke nguvu zetu katika timu gani ili kuendelea kutekeleza lengo letu kama kampuni la kushirikiana na serikali kwenye michezo liweze kutimia.”

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here