Home Kitaifa Ajib anawakosoa Simba na kurudi usingizini

Ajib anawakosoa Simba na kurudi usingizini

19342
0
SHARE

Na Gharib Mzinga

Hakuna shaka kitu kizuri hupendwa na wengi, lakini hakipendwi na wote. Katika kandanda kunasuala liitwalo ushabiki, ni kitu kizuri sana kuwepo, ushabiki unaleta ladha kamili na maana nzima ya soka. Ushabiki huu unapelekea watu kuamua kuukataa ukweli hata ukiwa upo wazi.

Hakuna haja ya ubishi, tukiweka ushabiki kando mshambuliaji wa Yanga Ibrahim Ajib ni miongoni mwa wachezaji wazuri wenye uwezo mkubwa sana katika ligi kuu Tanzania Bara. Hauitajiki kuwa shabiki wa Yanga ili kukubali hili.

Ajib ni mshambuliaji aliyelelewa katika kikosi cha vijana cha Simba SC, kabla hajapandishwa kikosi cha kwanza na baadae kutimkia katika klabu ya Yanga ambayo ni hasimu mkubwa wa Simba, kwa ada ya shilingi milioni 50 za kitanzania, alijiunga huko baada ya Simba kushindwana nae kimaslahi.

Kitendo cha Ajib kujiunga na Yanga kiliwakera sana wanamsimbazi, hali iliyopelekea Ajib asemwe sana kwa kauli mbali mbali zikiwemo, msaliti, mbinafsi, alikua ana mapenzi na Yanga kila aina ya mabezo alipatiwa. Simba wakajibu mapigo kwa kumsajili kiungo mashuhuri wa Yanga Haruna Niyonzima.

Ibrahim Ajib amekua akisemwa kwamba ni mvivu, mtegezi, hapendi kukaba na hafanyi mazoezi ya kutosha ndio maana alipokua na Simba hakua akimaliza dakika 90. Kauli hizi zimeandikwa na kusemwa na wadau wengi wa soka wanaomfahamu vizuri Ajib.

Kutokana na kudharauliwa, kuitwa garasa kutukanwa na kubezwa kwa hali ya juu, Ibrahim Ajib alipojiunga na Yanga aliamua kuwaonesha watu wanaomsema vibaya hususan washabiki wa klabu yake ya zamani kuwa yeye ana uwezo mkubwa na wamefanya makosa kumuacha.

Katika michezo ya awali ya ligi kuu Tanzani Bara, Ajib alicheza katika kiwango cha juu sana, akawa anafunga, anasaidia mabao mengi, hatari katika mipira ya kufa, ukitaka kuamini hilo kaangalie rekodi ya michezo sita ya mwanzo ya Yanga, alizinyanyasa timu kama vile Lipuli, Njombe Mji, Majimaji, Ndanda, Mtibwa na Kagera Sugar.

Ajib ambaye watu wengi walikua wakimtaka ndiye yule wa michezo ile sita ya awali, alifanya kila jambo uwanjani, aliibeba Yanga katika mabega yake, alifanya hivyo kwa kusudio la kuwaonesha Simba kuwa Ajib ni nani, hata katika mchezo dhidi ya Kagera akaamua kuwaonesha wapinzani jina lake na namba ya jezi yake kama alivyofanya Lionel Messi, Cristiano Ronaldo na Mauro Icard.

Laiti kama kile kiwango angedumu nacho naamini mwisho wa msimu huu Ajib angekuwa South Africa Mamelod Sundown, Orlando Pirates, Kaizer Chief, DRC Congo TP Mazembe, au Misri Zamalek, au Al
Ahly na huko angeitafuta vyema safari ya England, Italia, Ujerumani au Hispania.

Vyombo vya habari vya Tanzania vimemtangaza vilivyo Ajib wa Yanga, kuliko alivyokua Simba. Kuna baadhi ya watangazaji waliwahi kuchumpa mipaka kwa kumpa sifa za kutisha kama vile kushushwa kutoka mbiguni, pia mtoto wa Mungu. Ajib akajiona kama aliyeonja pepo, na aliamini ameshafanikiwa kuwakosoa Simba.

Baada ya mchezo wa Yanga dhidi ya Singida, Ajib ameshuka kile kiwango cha michezo sita ya awali, athari yake imekua ndogo, huwenda anajiamini udhaifu wa kikosi cha Yanga unamtia kiburi aone hakuna wakumuweka benchi, labda angekuwa bora kama angekutana ya Yanga ya moto wa gesi ikiwa na Msuva, Ngoma, Kamusoko, Niyonzima, Tambwe, Bosou, Dida, chini ya Hans van Pluijm lakini hawa wote hawapo katika utimamu kama wa miaka miwili iliyopita. Na wengine wameshaachana na klabu hiyo.

Ajib anaamini ameshaionesha Simba na wameshajutia juu ya kumuacha, hivyo amerudi katika kitanda chake kile kile alichokua analalia akiwa Simba ili aendelee na usingizi wake, nilichojifunza ni kwamba Ajib ana pande mbili za shilingi akiamua anafanya makubwa asipoamua atawaudhi. Siku njema.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here