Home Kimataifa Mourinho hafanani kabisa na wanaume wa Dar

Mourinho hafanani kabisa na wanaume wa Dar

10355
0
SHARE

Na Priva ABIUD.

Ukisema Mourinho sio kocha mzuri itabidi upelekwe moja kwa moja Mirembe hakuna haja ya kukupimwa akili. Bila shaka Mourinho ana heshima kubwa kwenye soka. Banafsi sipendi aina yake ya uchezaji lakini hilo halizuii kusifia mafanikio yake.  Lakini kuna kitu ambacho natamani kichunguzwe kwenye moyo wa Mourinho. Mourinho anapenda kisichopendwa na kinachopendwa Mourinho huwa hakijali sana. Huenda Mourinho akawa kama pilipili, mchungu lakini anahitajika kwenye chakula. Wakati Fulani Mourinho amekuwa na maneno matamu anapomtaka mchezaji lakini inapotokea anahitajika popote huwa hajali. Mara kadhaa ameruhusu baadhi ya wachezaji muhimu kuondoka au kuwasweka benchi.

Akiwa na klabu ya Inter Milan aliruhusu mchezaji Bora kabisa wa klabu hiyo kwa wakati ule Zlatan Ibrahimovic kutimkia klabu ya Barcelona. Mourinho alipohojiwa na waandishi wa habari alisema hakupendezwa hata kidogo na uhamisho wa Ibra. Aliongeza kuwa tumepoteza mchezaji bora na tumempata mchezaji bora (Samuel eto’o). Hata hivyo alipoulizwa kama aliweka juhudi kumzuia alisema “sikuwahi kujadiliana nae kuhusu hilo, wala sikumnyima yeye kuondoka, niliongea nae kabla hajafikia maamuzi yake lakini sikutaka kumshauri chochote”. Zlatani kwa wakati ule alikuwa kipenzi cha mashabiki wa Inter Milan baada ya kuwa mfungaji bora msimu wa 2008-09 akiwa na magoli 25, alikuwa mchezaji bora wa mwaka wa Italia Serie A, mchezaji bora wa kigeni kwa miaka miwili mfululizo.

Katika klabu ya Chelsea alimkuta Juan Mata akiwa katika kiwango bora kabisa msimu ule. Hakika alikuwa katika kipindi kizuri katika maisha yake ya soka. Mourinho hakujali nafasi ya Mata katika klabu ile na hatimaye alimpiga bei kwenda klabu ya Mann United. Bila shaka Mata alikuwa kipenzi cha mashabiki wote wa Chelsea. Alikuwa anajituma licha ya kuwa na mwili kama wa kwangu. Aliitumikia Chelsea kwa moyo wake wote. Hata wakati anaondoka hakuna mshabiki wa Chelsea aliyesimama na kumpigia Mourinho Makofi.

Mwaka huu amerudi kitendo kile kile alichofanya kwa Mata na Ibra. Amemuachia mkhitaryan ambaye mwanzo wa msimu huu alionekana kuwa na kiwango bora kabisa katika mechi za mwanzo. Mkhitaryan kabla ya kuja katika klabu ya Man united alikuwa na kiwango bora kabisa kule Bundasliga. Mahabiki wengi wa united walimpenda micky kutokana na uwezo wake, na alionekana kukubalika na mashabiki wengi wa United. Mourinho amemtoa kama mbuzi wa kafara ili kumpata Sanchez. hakuna shabiki wa Arsenal aliyekuwa tayari kumpoteza Sanchez kwa United, na hakuna mshabiki wa Man united aliyekuwa tayari kumpoteza Micky hasa kwa wapinzani wao Arsenal. Hapa ndipo Mouyrinho alipowashika kidevu amshabiki wa pande zote mbiuli.

Mourinho amepewa Cheni bandia ila ametoa hela feki. Walichokitaka mashabiki wa United ni Sanchez, lakini kinyonge wanampoteza mchezaji mpole na mtaratibu kabisa ambaye hakuwa na tatizo na mtu. Huyu ndiye Mourinho anakunyang’anya furaha anakupa tabasamu. Labda hukuelewa kichwa cha habari? Kumetokea wimbi kubwa sana la wanaume wa dar wanaogopa kuachana na wapenzi wao kisa tu ni wazuri au wana hela (Mario/Serengeti boys) yaani wao mwanamke wake akiwa mzuri yupo tayari hata kupiga magoti. Aliyewapa Moyo huo hakumpa Mourinho moyo kama wenu. Mourinho hajali wewe ni nani na una nini.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here