Home Kitaifa Simba, Yanga, zinaongoza kustaafisha wachezaji

Simba, Yanga, zinaongoza kustaafisha wachezaji

5626
0
SHARE

Kiungo wa zamani wa Simba amri Kiemba amefunguka kuwa, idadi kubwa ya wachezaji wa Tanzania wanastaafishwa na vilabu vya Simba na Yanga.

Ndio, Kiemba amethibitisha hilo kwakuwa wachezaji wengi hustaafu bila ridhaa yao lakini viongozi au kelele za mashabiki wa timu hizo huchangia kwa kiasi kikubwa wachezaji kuamua kustaafu huku wakiwa bado wanatamani kuendelea kucheza.

Mchezaji kama musa hassani mgosi alitangaza kustaafu soka kisha kupewa umeneja kwenye klabu ya Simba nafasi ambayo hakudumu nayo kwa muda mrefu akatolewa na kupelekwa kuwa kocha wa timu ya vijana lakini baadae akasajiliwa na Dodoma FC ya ligi daraja la kwanza kwa ajili bya kuitumikia kama mchezaji na sasa anacheza.

Inaelezwa NIco Nyagawa pia alistaafishwa Simba lakini hata Yanga kuna wahezaji ambao kwa sababu waliitumikia klabu hiyo kwa muda mrefu baada ya kuondoka mashabiki wanawapigia kelele kwamba ni wazee, Jerry Tegete na Mrisho Ngasa kwa sababu wameshacheza yanga kuondoka kwao kunafanya waonekane ni wazee kwa sababu tumezoea kuona wachezaji wakishacheza vilabu hivyo wengi mwisho wao huwa ni kustaafu.

Unapomzungumzia mchezaji kama Ramadhani Singano ‘Messi’ ni mchezaji aliyecheza timu ya vijana ya Simba pamoja na Mkude, Ndemla, Ajib lakini kwa kuwa yeye ameshatoka kwenye vilabu hivyo usishangae siku utakaposikia akiitwa mzee.

“Kwa sisi wachezaji tunavyojua, mchezaji anakuwa mkubwa akicheza Simba na Yanga. Cheza timu nyingine zote hata kwa misimu 20 lakini ukienda simba na yanga utaonekana bado kijana. Mchezaji anaonekana mzee akishacheza simba au yanga ndiyo maana wachezaji wa timu hizo ndio huwa wanastaafu lakini wale wa timu nyingine hawastaafu.”

“Unajua unapocheza Simba au Yanga watu wanakusikia, wanakuona na kusoma sana habari zako kwa hiyo inafika wakati wanakuchoka lakini ukiwa nje ya simba na yanga husikiki sana hadi timu yako inapokutana na simba au yanga lakini ukiwa mchezaji wa hivyo vilabu viwili hata ukienda mazoezini habari zako zinasikika.”

Kiemba amesema kuna wakati mchezaji anakuwa kwenye kiwango bora sana lakini kuna wakati anapitia kipindi kigumu ambacho kiwango chake kinapokuwa kimeshuka, nyota huyo wa zamani anasema hilo ni jambo la kawaida kwenye soka na halihusiani na mara nyingi halihusiani na umri wa mchezaji.

“Kwa mchezaji kiwango ni kitu cha kupanda na kushuka, inawezekana mashabiki wakakusikia kwa miaka miwili ukiwa katika kiwango cha juu halafu unapofika mwaka wa tatu kiwango kinakuwa kimeshuka hapo ndio unaonekana umezeeka kwa hiyo wanataka uondoke.”

“Mimi najua kwamba kiwango ni kitu cha kupanda na kushuka kwa hiyo kinaposhuka huwa sipati shida kwa sababu najua hiki ni kipindi cha mpito, unaweza ukacheza kwa kiwango cha juu hata kwa miaka mitano lakini itafika wakati unaweza ukashuka hata kwa miezi miwili, sasa wachezaji wengi ikifika wakati kiwango kimeshuka namna ya kurudi kwenye ubora wao ndio inakuwa shida.”

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here