Home Kitaifa TFF inatafuta wadau soka la ufukweni

TFF inatafuta wadau soka la ufukweni

1777
0
SHARE

Leo Januari 21, 2017 TFF imeendesha program maalumu ya maboresho ya timu ya Taifa ya soka la ufukweni.

Program hii imeanza ikijumuisha wachezaji 48 waliochaguliwa kutoka kwenye timu zilizoshiriki ligi ya vyuo vikuu mkoa wa Dar es Salaam na wachezaji wale waliokuwemo katika timu ya Taifa iliyoshiriki michuano ya Copa Dar es Salaam.

Program hii itakuwa chini ya mwalimu Boniface Pawasa na Deogratias Lucas na itakuwa inafanyika kila Jumapili kuanzia saa 9 mchana mpaka saa 12 jioni.

Lengo likiwa ni kuwaandaa wachezaji kwa ajili ya kujenga timu ya Taifa itakayoshiriki michuano ya kimataifa mwaka huu 2018.

Tunaomba kuchukua fursa hii kuwakaribisha wadau mbalimbali kutuunga mkono.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here