Home Uncategorized Dili la Sanchez bado kizunguzungu lakini leo…

Dili la Sanchez bado kizunguzungu lakini leo…

8916
0
SHARE

Wiki hii nzima ilikuwa ni mvutano kati ya Manchester United, Alexis Sanchez, Mino Raiola na Henrikh Mkhitaryan kuhusiana na usajili lakini hadi usiku wa Ijumaa hakuna lolote ambalo limetokea.

Jana kulikuwa na taarifa kwamba Henrikh Mkhitaryan ameaga Manchester huku akitoa machozi lakini United walichoka baada ya Sanchez kuonekana akiwa mazoezini na timu ya Arsenal.

Taarifa mpya za jana usiku zinasema kila kitu kimshakamilika na Alexis Sanchez naye ameshaaga Arsenal tayari kuelekea United uhamisho ambao unaweza kukamilika chini ya masaa 12 yajayo.

Lakini mkanganyiko zaido kuhusiana na Sanchez ni kwamba kocha Arsene Wenger anadaiwa kuweka jina lake katika kikosi ambacho kitacheza hii leo dhidi ya Crystal Palace.

Lakini tayari kwa habari za hii leo inaonekana 60% uhamisho wa Alexis Sanchez kwenda Manchester United unakwenda kutokea kutokana na ripoti nyingi za jana usiku kwamba nyota huyo ameshaondoka hotel aliyokuwa kwa ajili ya kwenda kukamilisha dili.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here