Home Kimataifa Tetesi za usajili barani Ulaya, Dzeko anarudi EPL?

Tetesi za usajili barani Ulaya, Dzeko anarudi EPL?

15457
0
SHARE

Klabu ya Chelsea inatajwa kuingia rasmi katika vita ya kumnunua mshambuliaji wa As Roma Edin Dzeko ambapo Chelsea wanajipanga kutoa £50m kwa ajili ya mshambuliaji huyo pamoja na mlinzi wa kushoto wa Roma Emerson Palmieri.

Juventus wanaonekana wamerudi katika klabu ya Arsenal na sasa wanataka kumchukua beki wao Hector Bellerin, Juventus wanatajwa kwamba wako tayari kutoa kiasi cha £40m kwa ajili ya kumnunua Bellerin.

Klabu ya Manchester United inatajwa kuanza mazungumzo na golikipa wao David De Gea ili kujaribu kumuongezea mkataba, United wanataka kumpa De Gea mkataba mpya ili kumzuia asiende Real Madrid.

Inadaiwa kwamba klabu ya Tottenham Hotspur imeingia katika vita na Manchester United kwa ajili ya kumsajili winga wa PSG Lucas Moura ambaye anatajwa kwamba siku zake kuitumikia PSG zimekaribia kuisha.

Jean Michael Seri kiungo wa Ivory Coast anatajwa kuwaweka vitani Chelsea, PSG na Manchester City ambapo vilabu vyote hivyo vitatu vinatajwa kuhitaji huduma ya kiungo huyo wa Nice.

Inadaiwa kwamba klabu ya Real Madrid iko mbioni kufanya kufuru katika soko la usajili ambapo wanatajwa kutaka kuwanunua Roberto Lewandoski, Neymar pamoja na Eden Hazard kutoka Chelsea.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here