Home Kimataifa Man United hesabu ni tatizo au kiburi?

Man United hesabu ni tatizo au kiburi?

15684
0
SHARE

Priva ABIUD

Hivi majuzi kuna mwenzenu alimfananisha Hazard na Lingard binafsi naheshimu sana afya za watu maana unaweza ukamtukana mtu ukasikia kalazwa. Nilichogundua baada ya Man united kukaa miaka mitano bila ubingwa, baadhi ya mashabiki wao wanapaswa wakafanyiwe mila makwao. Maana zisharuka sasa. Vile vijitabia tulivyoviona kwa mashabaiki wa Arsenal nishaanza kuviona kwao.

Takwimu zinasema Paul Pogba ni mbunifu kuliko Kelvin De Bruyne. Ni kweli namba hazidanganyi lakini kuna tofauti kubwa ya uwezo na takwimu. Inaonekana Pogba kumfikia KDB nafasi za kutengeneza  magoli kumefanya wengine wamuone ni mbunifu zaidi. Ubunfiu ni nini? Labda ni vionjo vya mbwembwe mguuni? Kama chenga, kanzu? Au ni nini? Kama ni hayo nakubaliana nao, kwamba Pogba ni mjuvi.
 
Lakini kama ni uwezo wa kuichezesha timu uwanjani, pasi muhimu, maamuzi ya mchezaji kwa wakati, ushapu wa kuandaa mashambulizi, kujiamini kwenye faida, KDB ni bora kuliko Pogba. Ni kweli pogba ametenegeneza magoli 9 sawa na KDB licha ya kwamba amemzidiwa michezo 10. KDB amecheza michezo 23 huku labile akicheza michezo 13. Kwa mantiki hii mashabiki wa Man united wanajificha kwenye mwamvuli huu wa mechi chache
 
Hivi Kwani kucheza mechi chache na kuwa na takwimu nzuri ndio ubora wa mchezaji? Nawauliza nyie mashabiki mnao kurupuka kila mkiona namba? Inaonekana mlifundishwa hesabu na mwalimu wa sarufi. Bila shaka wengi wenu mlifeli hesabu. Mnataka kuniaminsha kwamba, kwa kuwa Pogba amefunga magoli matatu kwenye mechi 13 na kutengeneza magoli 9, hivyo akicheza tena mechi nyingine 13 atafikisha idadi hiyo hiyo?
 
Jifunzeni kuweka akiba ya maneno mara moja hii mshasahau Mkhitaryani mechi tatu za mwanzo alitengeneza magoli 5 leo yupo wapi? Hatupimi kina cha maji kwa upana wa bwawa.
 
Pogba msimu huu amekosekana kwenye mechi ngumu na muhimu za United. De Bruyne amecheza karibia kila dakika kwenye kikosi cha City. Maana yake ni kwamba De Bruyne amepita kwenye milima na mabonde. Njia ndefu ina mengi. Pogba baadhi ya mechi ngumu na muhimu hakuwepo. Kingine Pogba ni mchezaji anayetegemea zaidi ufanisi wa klabu yake ili afanye vizuri. Yaani ili Pogba acheze vizuri anahitaji zaidi timu yake icheze vyema. Huenda ukatamani kunitukana. Naomba nikukumbushe maneno yenu ya msimu uliopita. Mlisema Pogba anshindwa kucheza vyema kwa sababu gani? Pogba akicheza chini ya kiwango lawama mlikuwa mnatupia Pogba au Mourinho? Nyie si mlikuwa mnasema hakuna  wachezaji sahihi wa kumzunguka Pogba?.
 
Au nawasingizia nyie? Nyie si mlisema mnahitaji watu kama Vidal na Marchisio? Nyie nyie si ndio mliosema Pogba alicheza vyema Juventus kwa sababu alizungukwa na watu?
 
Man city inamhitaji KDB ili ipate matokeo chanya. Yaani bila debruyne Man city haifanyi vizuri sana. Timu imejengwa chini ya Debruyne. Pogba anaitegemea Man United icheze vyema. Takwimu za Pogba wetu hizi hapa. Mchezo mgumu pekee aliyoicheza ni dhidi ya Arsenal. Hongera kwake aliweza kutengeneza magoli mawili. Michezo aliyofunga ni michezo dhidi ya West Ham ambapo United ilishinda goli 4 mchezo mwepesi kabisa, mchezo mwingine ni dhidi ya Swansea Vibonde nayo, United ilishinda magoli 4 na mchezo huo huo alitengeneza goli 1.  Akakosekana michezo dhidi ya Liverpool, Spurs na Chelsea. Mchezo dhidi ya Newcastle alifunga goli 1 na alitenegeneza goli 1 mchezo ambao United ilishinda magoli 4. 
Mchezo dhidi ya Everton na Stoke city alitenegeneza magoli mawili. Katika michezo 13 aliyocheza ni michezo 6 ambayo hakufanya chochote uwanjani. Katika ichezo hiyo sita, united ilishinda Mitatu na kutoka suluhu miatatu. Katika michezo hiyo mitatu United ilicheza chini ya kiwango kabisa na Pogba akashindwa kusiamamia shoo, nmesema hapo awali bila United kufanya vizuri Pogba huwezi kumuona kwenye matokeo. Pogba hajafunga goli lolote lililoipa timu ushindi
 
Turudi kwa Debruyne. KDB alifunga magoli michezo ifuatayo, dhidi ya Chelsea ambapo walishinda goli moja, dhidi ya Arsenal ambapo alifunga goli moja kati ya matatu, dhidi ya Spurs ambapo walishinda magoli manne, dhdi ya Southampton ambapo waloishinda goli 2, dhidi ya  Leicester ambapo alifunga goli 1 kwenye ushindi wa goli 2, pia aliwafunga Swansea. Ametengeneza magoli mawili kwenye mechi ya Liverpool,  Amefunga magoli ya ushindi mawili tu.
 
HitimishoKatika michezo 13 pogba aliyohusika aidha kwa kutengeneza goli au kufunga amefanya vyema michezo 7 nusu ya michezo yote aliyocheza. Hivyo hivyo kwa Deburyne amefanya vyema mechi 13 kati ya 23 ni zaidi ya nusu ya michezo. Kufikia hapo mimi niseme tu, Debruyne ndiye kiungo mshambuliaji Bora zaid England kwa sasa akiwa ametengeneza nafasi 67 za magoli, Krosi 148, mipira ya kupitisha mara 24. Pia Pogba ndiye kiungo wa katikati bora yaani namba kwa sasa. Takwimu zake ni kubwa ukilinganisha na viungo wengine wanaocheza dimba la kati. Umuhimu wake wakati timu ikiwa kwenye kiwango bora unaonekana. Ni mchezaji ambaye anaweza kubeba jukumu mengi. Ila kuniambia ni bora kuliko De bruyne ni kuniaminisha maji ya kidumu ni mengi kuliko ya kwenye Ndoo.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here