Home Kitaifa Yanga imesaini mkataba wa zaidi ya bilioni 2

Yanga imesaini mkataba wa zaidi ya bilioni 2

6081
0
SHARE

Leo Jumanne Januari 16, 2018 klabu ya Yanga imeingia mkataba wa miaka mitatu (3) na kampuni ya utengenezaji wa vifaa vya michezo ya Macron ambayo makao makuu yake yapo nchini Italy, Macron watakuwa ndio watengenezaji wakuu wa vifaa vyote michezo vya klabu hiyo.

Katibu mkuu wa yanga Charles Boniface Mkwasa amesema, mkataba huo unathamani ya Tsh. 2 Bilioni ambapo kutakuwa na ongezeko la asilimia kila mwaka kutokana na mauzo ya jezi na vifaa mbalimbali.

mwakilishi wa kampuni ya Macron Tanzania Bw. Suleyman Kareemamesema, wamevutiwa na Yanga kwa sababu ni klabu nchini hivyo itakuwa vizuri kufanya kazi na klabu hiyo.

“Sisi Macron tuna project kubwa hapa Tanzania tumeshaingia mkataba na shirikisho la soka la Tanzania (TFF) na mambo yanaendelea vizuri, tumeona pia Yanga ni klabu kubwa itakuwa vizuri kufanya nao bishara ndio maana tukaamua kuja kuwapa mpango ngazi wetu na wao wakakubali, kwa sasa kila kitu kinaenda sawa”-Suleyman Kareem, mwakilishi Macron Tanzania.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here