Home Kitaifa Watano Yanga kuikosa Mwadui

Watano Yanga kuikosa Mwadui

4829
0
SHARE

Klabu ya Yanga itawakosa nyota wake watano kwenye mchezo wa ligi kuu Tanzania bara utakaochezwa Jumatano Januari 17, 2018 kwenye uwanja wa uhuru, Dar.

Afisa habari wa klabu hiyo Dismas Ten amewataja wachezaji hao ambao wataukosa mchezo huo kutokana na sababu mbalimabi ikiwemo kuumwa na majeraha ambayo yanawakabili baadhi ya wachezaji.

“Donald Ngoma na Geoffrey Mwashiuya hawatakuwa sehemu ya mchezo wa kesho dhidi ya Mwadui, Mwashiuya anaumwa lakini Ngoma bado anaendelea kuuguza majeraha, Kamusoko na Abdallah Shaibu ‘Ninja’ pia bado hawajawa sawasawa ingawa Kamusoko tayari ameanza mazoezi taratibu baada ya kutoka kwenye majeraha makubwa”-Dismas Ten, afisa habari Yanga.

“Tambwe amerejea, amepona malaria iliyokuwa inamsumbua, leo amefanya mazoezi kwa hiyo benchi la ufundi litaangalia kama wataweza kumtumia mchezaji huyo.”

“Maandalizi yote yamekamilika na tuko tayari kwa mchezo kuhakikisha kwamba tunapata matokeo kwa ajili ya kutetea ubingwa wetu.”

Ukiachana na wachezaji hao wanne ambao wataukosa mchezo huo kutokana na sababu za majeraha na kuumwa, Obrey Chirwa yeye ataukosa mchezo huo akiwa anatumikia adhabu yake ya kufungiwa mechi tatu na TFF baada ya kubainika kumpiga mchezaji wa Tanzania Prions november 25, 2017 wakati wa mchezo wa ligi kuu kati ya Yanga dhidi ya  Prisons kwenye uwanja wa Azam Complex.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here